Thursday, July 28, 2016

MAJALIWA AKABIDHIWA MADAWATI KWA AJILI SHULE ZA DAR ES SALAAM LEO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na wananchi wa Temeke baada ya kuwasili kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi kukabidhiwa madawati na fedha shilingi milioni 100  kwa ajili ya Shule za Dar es salam  Julai 28, 2016. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. (Picha na Oisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa na Balozi wa Kuwait  nchini, Jaseen Al Najem  na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msigi ya Chamazi wakiwa wamekaa kwenye  madawati mawili kati ya 300 yaliyotolewa na Kuwait ili kukabiliana na tatizo la madawati jijini Dar es salaa. Makabishianoni hayo yalifanyika kwenye  Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salaam Julai 28, 2016. Waliosimama watatu kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, , Augustine Mahiga, Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje  na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Susan Kolimba na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru , Murtaza Adamjee wa Jumuiya ya Mabohora nchini baada ya kukabidhiwa madawati 105 kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salam Julai 28, 2016. Kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini, Jaseem Al Najem na Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Susan Kolimba. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)

 Baadhi ya wanafunzi na mmoja wa wananchi waliohudhuria hafla ya kukabidhi madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa Waziri Mkuu kwenye shule ya Msingi yaChamazi jijini Dar es salaam Julai 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru , Murtaza Adamjee wa Jumuiya ya Mabohora nchini baada ya kukabidhiwa madawati 105 kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salam Julai 28, 2016. Kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini, Jaseem Al Najem na Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Susan Kolimba. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya  Chamazi jijini Dar es salaam baada ya kuwasili shuleni hapo kukbidhiwa madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa ajili ya Shule za Dar es salaam  Julai 28, 2016.Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam, Theresia Mmbando, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Mkuu wa wilaya ya Temeke  Felix Lyaviva. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu