Na Shamimu
Nyaki WHUSM
Serikali
kupitia Jeshi la polisi limewaasa vijana nchini kushiriki katika michezo
mbalimbali ya kuigiza yenye lengo la kutoa elimu kwa jamii ili iweze kupambana
na kuzuia uhalifu.
Wito
huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Inspekta Salum Abdalah kutoka Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi alipokuwa akitoa mafunzo kwa vijana kuhusu Umuhimu wa
kutoa elimu kuhusu kuzuia na kupambana na uhalifu nchini kupitia michezo ya
kuigiza.
Inspekta
Salum amesema kuwa miongoni mwa mikakati ya serikali ni kuwajengea vijana uwezo
wa kuwa na tabia njema na kupata kipato cha halali kwa kuwawezesha kupata
mafunzo ya stadi za kazi kwa lengo la kuimarisha na kukuza uchumi, pamoja na
kuwapa uwezo wa kuendeleza vipaji vyao.
“Ili
kuwawezesha vijana kuwa na tabia njema na kuwa na maadili yanayotakiwa hatuna
budi kuanzisha mbinu za kuwawezesha
kuanzisha vikundi vya ujasiriamali, ulinzi shirikishi na kuwepo kwa mipango
thabiti wa kushiriki katika mafunzo, semina na warsha mbalimbali”. Alisema
Inspekta Salum.
Inspekta
Salum ameongeza kuwa wananchi ,wadau pamoja na mamlaka zinazohusika na
maendeleo ya Vijana, Michezo na ujasiriamali kuwahamasisha vijana ili waweze kujshughulisha na shughuli zinazoleta maendeleo kwa taifa na
kujiepusha katika vitendo vya uhalifu.
Mmoja
wa washiriki wa mafunzo hayo Bw Ismael Mnikite
amesema mafunzo hayo yamemuwezesha kuelewa umuhimu wa ulinzi
shirikishi kwa vijana kwakua anaamini ndio wenye uwezo mkubwa wa kushawishi jamii
kujiepusha na vitendo viovu.
“Mafunzo
haya yameniwezesha kuelewa umuhimu wa kuwa mfano kwa jamii kwani nitatumia elimu hii kupanua
uwezo wa kutafuta miradi itakayoniwezesha kupata mikopo kutoka kwa wawezeshaji ili nisipate tamaa ya
kujiingiza katika uhalifu”.Alisema Bw. Ismael.
Mafunzo
hayo yameandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana ili kuwasaidia vijana kuwa
raia wema na kushiriki ipasavyo katika shughuli za ujasiriamali na ulinzi wa
jamii kwa kutumia elimu na vipaji walivyonavyo.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment