2


SI LA KULIKOSA

Friday, July 22, 2016

Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akutana na uongozi wa Radio Maarifa iliyopo Jijini Tanga


Mkurugenzi na mmiliki wa wa Redio Maarifa Bw. Mohamed Somji akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mazungumzo kuhusu kupata masafa ya kurusha matangazo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kushoto ni mtangazaji na mchambuzi wa mada katika Redio hiyo Sheikh Jalala leo Julai 20, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akizungumza  na uongozi wa Redio Maarifa kuhusu kupata masafa ya kurusha matangazo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo Julai 2016, wa pili  kushoto ni Mkurugenzi na mmiliki wa wa Redio Maarifa Bw. Mohamed Somji na kushoto ni mtangazaji na mchambuzi wa mada katika Redio hiyo Sheikh Jalala.

Mkurugenzi na mmilikiwa wa Redio Maarifa Bw. Mohamed Somji akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura Ofisini kwa Naibu Waziri kuhusu kupata masafa ya kurusha matangazo kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es Salaam leo Julai 2016.

Mkurugenzi na mmilikiwa wa Redio Maarifa Bw. Mohamed Somji akimuonesha Naibu Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura baadhi ya nyaraka za kibali cha awali cha kurusha matangazo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisini kwa Naibu Waziri leo Jijini Dar es Salaam Julai 20, 2016.

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu