Na
Raymond Mushumbusi WHUSM
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kupambana
na wale wote wanaojihusisha na wizi wa kazi za wasanii na kuzisambaza kinyume
cha sheria.
Mhe.
Nape Nnauye ametoa ahadi hiyo mbele ya wasanii na wadau wa sanaa wakati
akizundua filamu ya Sikitu na kuahidi kutochoka kupambana katika vita dhidi ya
wezi wa kazi za wasanii wa filamu na sanaa kwa ujumla.
“Nataka
niwahakikishie wasanii na watengeneza filamu Tanzania kazi hii nimeianza na
nitaendelea nayo na hatutoshindwa tutashinda na nawaonya wanaofanya kazi ya
kuiba kazi za wasanii waache mara moja” alisema Mhe. Nnauye.
Mhe.
Nnauye ameongeza kuwa Serikali itaendelea kujenga misingi mizuri kwa wasanii na
tasnia ya filamu Tanzania na kuhakikisha wasanii na watayarishaji wanapata
mitaji itakayowawezesha kuzalisha filamu
bora na kupata masoko mazuri.
Aidha
amewaomba wadau wa sanaa na filamu kwa ujumla kukaa na Serikali na kuangalia
namna bora ya kurasimisha vibanda vinavyoonesha filamu za kitanzania kuwa kumbi
maalum kwa ajili ya kuonesha filamu hizo ili kuongeza soko la filamu hizo
kupitia kumbi hizo.
Kwa
upande wake katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo amewapongeza
watayarishaji wa filamu hiyo kwa kuzingatia maadili na wazidi kutengeneza filamu
zenye ubora zaidi ili kukuza tasnia ya filamu nchini.
Filamu
ya Sikitu imetayarishwa na kutengenezwa na Kajala Entertainment na imehusisha wasanii wengi
wenye uwezo mkubwa akiwemo Taiya, Mutrah, Jada, Asha Boko, Hemed Suleimani,
kajala Masanja, Amir Athuman ‘King Majuto’ na wengine wengi, imeandikwa na
kuongozwa na Leah Richard Mwendamseke na itaoneshwa katika
kumbi za sinema kwa muda wa siku saba kabla ya kuingia sokoni.
0 comments:
Post a Comment