Na
Mwandishi Wetu Dodoma.
Mapema
Septemba 2016 kwa mara ya kwanza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye aliwasilisha kwa mara ya kwanza Bungeni Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari na
kuanza kujadiliwa na kutolewa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa Habari
nchini.
Kwa sasa
Muswada huu unaendelea kujadiliwa na kuchambuliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Huduma na Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Peter Serukamba
na baada ya mchakato huo kukamilka utapelekwa kwa ajili kuanza kujadiliwa na
wabinge.
Sasa
hoja yangu naielekeza katika kuangalia Muswada huu hasa katika sehemu ya Tatu (c)
Uthibitishwaji wa wanahabari kifungu cha 18 (1) na (2) vinaelezea kuwa Mtu
hataruhusiwa kufanya kazi za uandishi wa habari isipokuwa kama mtu
amethibitishwa na Sheria hii na (2) inasema mtu ambaye anakusudia kufanya kazi
ya uandishi wa habari ataomba kuthibitishwa na Bodi kwa utaratibu wa maombi
utakaoainishwa katika kanuni.
Ukisoma
kifungu hiki na sehemu zake zote utaona kuwa lazima kutakuwa na vigezo ambavyo
mwandishi wa habari atapaswa kuwa navyo ili Bodi iweze kumthibitisha kuwa
mwandishi wa habari kamili na baadae kumpatia Press Card.
Tukiangali
kwa mifano tu ya taaluma ambazo watu wake wanapata udhititisho kutoka kwa Bodi
zao utaona kuwa hata vigezo vyenye ngazi fulani ya kitaaluma na kwa mfano wanasheria ili
kudhititishwa kuwa mwanasheria na kupata mhuri wa kuwa Wakili unabidi uwe na
Shahada ya Kwanza ya Sheria na kufanya baadhi ya mitihani ya kufuzu ili
kudhitishwa.
Kwa
waandishi wa Habari pia tutegemee kuwepo kwa vigezo na masharti ambayo kwa
vitahitaji kuongeza elimu tulizonazo katia fani yetu na pia hili litasababisha
sasa vyuo vya uandishi wa habari na mawasiliano kutoa elimu iliyo bora zaidi
ili kuendana na mabadiliko haya.
Tumeshudia
uwepo wa vyuo vya uandishi wa habari kila sehemu hata vingine ukiangalia
mazingira yake lazima utilie shaka kama vinatoa ile elimu inayostahili na
iliyodhibitishwa na mamlaka zilizopo za TCU na NACTE.
Niwaombe
tu wahusika katika vyuo vya uandishi wa habari kuzingatia vigezo na masharti ya
utoaji wa elimu ya Habari na Mawasiliano katika vyuo vyao kwani kuja kwa Sheria
ya Huduma za Habari ni mwanzo wa kuifanya taaluma ya habari kuwa taalum
inayoheshima na kuwa taaluma inayoheshimika sana na sio rahisi kuipata kama sasa watu
wanavofikiria tu ukitaka kuwa mwandishi wa habari unaweza kusoma miezi mitatu hivi basi
umekuwa mwandishi wa habari.
Ingawa
kuna baadhi watu wanasema wanatumia vipaji vyao vya uandishi wa habari na
utangazaji lakini tujue kuwa kipaji bila ya kuendelezwa ni kazi bure tunahitaji
kuviendeleza vipaji hivyo kwa kupata elimu na ujuzi zaidi wa fani ya habari ili
kuendana na mabadiliko ya teknlolojia na Sheria za nchini.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment