Ni baada ya muda mrefu mpendwa wetu,
Fatuma Salum kuwa katika safari huko Mozambiki katika kutafuta maisha,
ametutoka Duniani akiwa katika maandalizi ya kurudi nyumbani kwao kuiona
familia yake na Mzazi wake na ndugu zake waishio Kinondoni maeneo ya
Mkwajuni Jijini Dar es Salaam, ambapo siku mbili nyuma ameugua ugojwa
wa kuishiwa nguvu mkono na mguu upande mmoja na kukimbizwa Hospitali na
akiwa Hospitalini hapo alipata bahati ya kuongea na mama yake Mzazi na
baada ya hapo tulipata taarifa ya kuwa amefariki akiwa katika maandalizi
ambapo Ijumaa hii iliyopita alitarajia aanze safari na Ijumaa hiyo
hiyo mchana akaaga Dunia , hadi sasa wafanya biashara wenzake kwa
kushirikiana na familia ya mpendwa wetu mwili utalala Boda na asubuhi
safari itaanza, Familia ya mpendwa wetu inatowa asante kwa wote
walioshiriki kufanikisha michango yao na kujinyima ili kufanikisha
safari ya mpendwa kurudishwa nyumbani na wote wanao endelea kutowa pesa
zao na mawazo yao. shukrani ziwafikie wafanya biasha wenzake na
Madaktari wote na ndugu na jamaa kwakufanikisha taratibu za maandalizi. (KAZI YA MUNGU)
0 comments:
Post a Comment