WALIPEWA WIKI MOJA
KUTOA MAONI, BADO WANADAI MUDA ZAIDI.
MWENYEKITI KAMATI
ASEMA KWA MIAKA MINGI WAMEKUWA WAKIKWAMISHA MUSWAADA HUO.
Na
Mwandishi Wetu Dodoma
Wadau
wa habari nchini wameendelea kukacha kuudhuria kikao cha Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na hata kutoa maoni yao licha ya kupewa
barua za mwaliko na kuongezewa siku kumi za ziada kuwasilisha maoni yao kuhusu
Muswaada wa Sheria ya Huduma za Habari.
Akizungumza
katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii
wakati akifungua kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati Huyo Mhe. Peter Serukamba
amesema kuwa wao kama Kamati wanaendelea na kazi ya kisheria ya kutunga Sheria.
Ameongeza
kuwa wadau walikuja kwa mara kwanza mbele ya kamati na kupewa nafasi ya kutoa
maoni yao kuhusu Muswaada lakini walisema muda mchache wanahitaji muda zaidi wa kuusoma Muswaada na kuto amaoni yao.
Mhe.
Serukamba amesisitiza kuwa hii imekuwa tabia ya wadau walio wengi kila Muswaada
huu unapoletwa Bungeni wamekuwa wakisema hawako tayari na kuomba utolewe
Bungeni.
“Kwa
miaka 23 Serikali imekuwa ikiwasikiliza wadau mpaka mwaka jana Muswada uliletwa
Bunge lakini wakataa na kutaka urudishwe na kwa sasa wamerudia tena na sisis
kama Kamati tutaendelea na kazi yetu ya kutunga Sheria kwa kuzingatia maoni yaliyotumwa”
alisema Mhe. Serukamba.
Aidha,
kwa kuzingatia Kanuni za Bunge mara baada ya Muswaada kusomwa kwa mara ya kwanza
ni jukumu la wadau kuusoma Muswaada kwani unakuwa wazi kwa umma kwa ajili ya kuusoma
na kutoa maoni yao ili kuuboresha Muswaada husika.
Mhe.
Serukamba amewataja wadau walikokiri kupata barua ya mwaliko lakini bado hawakuweza
kuwasilisha maoni yao wala kufika kwenye kamati yake kama walivyoomba kuongezewa muda
wa kutoa maoni na bado wanasema Muswaada unahitaji muda zaidi ili waweze
kuusomwa Muswaada na kutoa maoni yao.
Amewataja
wadau hao kuwa ni, Pili Mtambalike, Legal and Huma Rights Centre, Union of
Tanzania Press Club, na Media Council of Tanzania (MCT).
Baadhi
ya wadau mmoja mmoja na kwa vikundi wamewasiliasha maoni yao katika Kamati hiyo
kwa njia ya barua pepe wakiwemao Chama cha wanasheria wa Tanganyika (Tanganyika
Law Society (TLS)).
Kamati
ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imekutana leo Oktoba 29
kupokea maoni ya wadau wa habari nchini ili kuendelea na maboresho ya Muswada
huo kabla ya kupelekwa kujadiliwa Bungeni.
MWISHO.
WAZIRI WA HABAR
0 comments:
Post a Comment