Sunday, November 6, 2016

Afrika nyuma ya Mahrez
 Mchezaji Bora Fifa 2016

LONDON, England
LICHA ya Riyad Mahrez kuingia katika kinyang'anyiro cha Mchezaji Bora wa Fifa pamoja na wakali kama Sergio Aguero, Gareth Bale, Cristiano Ronaldo, Antoine Griezmann Mesut Ozil  na Lionel Messi, ndipo macho ya Waafrika yalipotegwa.
Nyota huyo wa Kimataifa wa Algeria Mahrez (25), ametangazwa kuingia katika kinyang'anyiro hicho, na ndiye ambaye anaweza kuipeperusha bendera ya Afrika katika tuzo hizo kutokana na mafanikio makubwa aliyoipa Leicester City.
Mahrez, N'Golo Kante na Jamie Vardy ambao wote wamejumuishwa katika tuzo hizo, waliisaidia Leicester City kutwaa ubingwa wa Premier League msimu uliopita.

Mashabiki watapewa nafasi ya kupiga kura baada ya Fifa kujitenga na na Ballon d'Or mapema mwaka huu, huku wanafainali watatu wakitangazwa Desemba 2, mwaka huu.

Mchezaji Bora wa Fifa kwa Wanaume ni kati ya tuzo nane zitakazotolewa siku hiyo za Wacheza Soka Bora.

Kura za makocha na manahodha wa timu za taifa zitachangia asilimia 50 ya matokeo wakati wakati mashabiki nao wakiwa na nafasi ya kupiga kura pamoja na vyombo vya habaro zaidi 200 duniani.

Wachezaji kutoka Ligi Kuu England walioingia katika orodha ya wachezaji 23 watakaowani tuzo ya Mchezaji Bora wa Fifa 2016 itakayotolewa Januari 9, mwakani ni pamoja na Sergio Aguero, Kevin de Bruyne (Manchester City), Alexis Sanchez, Mesut Ozil (Arsenal), Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic (Manchester United) na Dimitri Payet (West Ham).
Wengine ni Gareth Bale (Real Madrid), Gianluigi Buffon (Juventus), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Andres Iniesta (Barcelona), Toni Kroos (Real Madrid), Robert Lewandowski (Bayern Munich),  Lionel Messi (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid), Manuel Neuer (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid), Alexis Sanchez (Arsenal) na Luis Suarez (Barcelona)

%%%%%%%%%

Gabon yamtimua kocha
Libreville, Gabon
MAANDALIZI ya Gabon kuelekea michuano ya Mataifa ya Afrika 2017, yameingia 'mchanga' baada ya kumtimua kocha wao Jorge Costa ikiwa ni miezi miwili kabla ya kitimtim hicho kuanza katika ardhi yao.

Kwa mujibu wa tovuti ya Shirikisho la Soka Gabon, mikoba ya Costa imebebwa kwa muda na Mkurugenzi wa Ufundi, Jose Antonio Garrido.

Hakuna sababu yoyote iliyotolewa kwa kufutwa kazi kocha huyo ambaye ni beki wa zamani wa timu hiyo aliyeteuliwa Agosti mwaka huu.

%%%%%%%%

Gyan kuikosa Misri
kufuzu Dunia 2018

ACCRA, Ghana,
MSHAMBULIAJI wa Ghana, Asamoah Gyan atakosa mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Misri Novemba 13, mwaka huu.

Nhidha huyo wa 'Black Stars' hatarajiwi kupona haraka majeraha aliyoyapa wakati akifanya mazoezi na klabu yake Al Ahli ya Falme za Kiarabu Jumanne iliyopita.

Gyan (30), ambaye ni mfungaji wa wakati wote Ghana akiwa na mabao 48, amekuwa akikabiliwa na majeraha ya mara kwa mara katika kipindi cha hivi karibuni. Kocha wa Black Stars, Avram Grant  alikuwa na matarajio ya kuwa na mchezaji huyo katika mbio za kushinda mechi hiyo.

%%%%%%%%

Gervinho kuikosa Afcon

Abidjan, Ivory Coast
HOFU imetanda kuwa huenda Gervinho akazikosa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani huko Gabon baada ya kumia viungio vya goti.

Majeraja hayo tayari yamemweka Gervinho nje katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 wakati Ivory Coast itakapoivaa Morocco Novemba 12 na mechi ya kirafiki dhidi ya Ufaransa siku tatu baadaye.

Nyota huyo wa zamani wa Arsenal aliumia wakati akiichezea klabu yake ya Hebei Fortune ya China.

rekodi Europa League
Mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Aritz Aduriz amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano katika mechi moja kwenye Europa League baada ya kufanya hivyo wakati wakiibuka na ushindi wa 5-3 dhidi ya Genk anayoichezea Mtanzania Mbwana Samata.

%%%%%

KIPIGO cha mabao 2-1 kutoka kwa Fenerbahce, kinainya Manchester United kwa mara ya kwanza katika historia yake kupoteza mechi tano mfululizo ugenini kwenye mchuano ya Ulaya. Novemba 3, 2016 imepigwa na Fenerbahce 1-2, Septemba 15 ikachwapwa 1-0 na Feyenoord 0-1, Machi 10 Liverpool iliipiga 2-0, Februari 18 ikakubali kulala 2-1 dhidi ya Midtjylland huku Desemba 8, 2015 ikitandikwa na Wolfsburg 3-2.

%%%%%

BALA AFUNGA KWA KUSHOTO
KWA mara ya kwanza Gareth Bale alifunga bao kwa kutumia mguu wa kushoto akiwa nje ya boksi sekunde ya 58 tangu mechi ilipoanza na kulifanya bao hilo kuweka rekodi ya kuwa la mapema zaidi kwa Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wakitoka sare ya 3-3 ugenini dhidi Legia Warsaw ya Poland wiki iliyopita.

%%%%%
LICHA ya Leicester City juzi kushindwa kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kulazimishwa sare tasa na Copenhagen, lakini imevunja rekodi ya michuano hiyo.
Sare ya 0-0 na miamba hiyo ya  Denmark, inawafanya Leicester kuwa timu ya kwanza katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kumaliza mechi nne za kwanza bila kuruhusu bao.
Ni Parma pekee iliyofanikiwa kufanya hivyo mwaka 1997-98, huku Malaga katika msimu wa 2012-13 ikiishia mechi tatu za mwanzo, lakini rekodi yao hiyo sasa ikitwaliwa na vijana wa kocha Claudio Ranieri.
Hata hivyo, shukrani kwa Leicester hazina budi kumwendea kipa wao, Kasper Schmeichel aliyeinyima klabu ya nyumbani kwao ushindi baada ya kuokoa ‘mchomo’ wa Andreas Cornelius katika dakika za mwisho.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu