Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2016 umebaki kuwa ni asilimia 4.5 kama ilivyo mwezi Septemba 2016.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Takwimu
za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ruth Minja wakati
akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo.
"Hii inaamanisha kuwa kasi ya upandaji
wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2016
imekuwa sawa na kasi ya upandaji wa bei ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia
mwezi Septemba 2016" alisema Minja.
Minja alisema fahirisi za bei zimeongeza
hadi 103.17 mwezi Oktoba, 2016 kutoka 98.72 mwezi Oktoba 2015 ambapo
mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Oktoba
2016 umebaki kuwa asilimia 6.0 kama ilivyokuwa mwezi Septemba 2016.
Alisema mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba
umechangiwa na kuongezeka kwa kasi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizi
za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba 2016 zikilinganishwa
na bei za mwezi Oktoba 2015.
Akizungumzia uwezo wa shilingi 100 ya
Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 96 na senti
92 mwezi Oktoba 2016 ikilinganishwa na shilingi 97 na senti 04
ilivyokuwa mwezi Septemba 2015.
Aidha akizungumzia hali ya mfumuko wa
bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki alisema nchini Kenya mfumuko
wa bei wa mwezi Oktoba 2016 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.47 kutoka
asilimia 6.34 mwezi Septemba 2016.
Alisema nchini Uganda mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba 2016 umepungua hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 4.2 mwezi Septemba 2016.
0 comments:
Post a Comment