Spika wa bunge mstaafu, Samwel Sitta,
au kama alivyojiita "Mzee wa Speed na Viwango" amefariki dunia usiku wa
kuamkia leo akiwa nchini Ujerumani alikopelekwa kupatiwa matibabu.
Taarifa iliyotolewa na mwanaye Benjamin Sitta, ambaye ni Meya wa
Manispaa ya Kinondoni, mapema leo aimethibitisha kifo cha Mzee Sitta.
Tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi spika wa bunge Job Ndugai,
kufuatia kifo cha mzee Sitta. Kwa muda mrefu Mzee Sitta ambaye aliwahi
kutumikia nyadhifa mbaklimbali tangu serikali ya awamu ya kwanza,
alikuwa haonekani hadharani kutokana na kuugua. Ni miezi michache
iliyopita Mzee Sitta alikuwa akionekana kwenye vyombo vya habari
akitembeelwa na viongozi mbalimbali kumjulia hali. Munhu aiweke roho ya
marehemu mahali pema peponi AMIN.
Mzee Sitta akiwa na mkewe, Mamam Margaeth Sitta wakati wa uhai wake
Spika sitta, akipokea ripoti maarufu ya
Richmond, kutoka kwa mwenyekiti wa kamati teule, Dkt. Harrison
Mwakyembe. Ripoti hii ilimuondoa madarakani aliyekuwa Waziri Mkuu wakati
wa kuingia kwa serikali ya awamu ya nne, Edward Lowassa.
Mzee Sitta alikuwa rafiki wa kila mtu. Hapa akiwa na Mbunge Tundu Lissu kutoka CHADEMA
Spika Sitta, akila kiapo cha kushika uspika wa bunge, mwanzoni mwa serikali ya awamu ya nne
0 comments:
Post a Comment