Mkazi wa Kijiji cha Ndubi kilichopo
wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Julius Mwambola (kulia), akionyesha
migomba iliyoangushwa kutokana na mvua iliyonyesha wilayani humo
mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni mke wake Nabwike Swebe.
Migomba ikiwa imeanguka kutokana na mvua hizo.
Mwanahabari Dotto Mwaibale, akichukua taarifa ya athari ya mvua hiyo kutoka kwa mkazi wa Kijiji cha Ndubi, Ambokile Mwangosi.
Nyumba ya Kikongwe, Gwanaloli Ndapapa ikiwa imeezuliwa paa na mvua hiyo ya upepo.
Kikongwe Maria Kamendu (85), akiwa
ameshika paa la nyumba ya jirani yake Gwanaloli Ndapapa iliyobomolewa
na mvua iliyonyesha mwishoni mwa wiki katika Kijiji cha Ndubi wilayani
Rungwe mkoani Mbeya na kuharibu migomba na baadhi ya nyumba.
Dotto Mwaibale, Mbeya
WAKAZI wa Vijiji vya Ndubi, Mpuguso Kata
ya Kisondela Tarafa ya Pakati wilayani Rungwe mkoani Mbeya wameathiriwa
na mvua kubwa iliyoambatana na upepo ambayo imeezua baadhi ya mapaa ya
nyumba na kuangusha migomba.
Akizungumza kuhusu tukio hilo mkazi wa
Kijiji cha Ndubi, Ambokile Mwangosi alisema wamepata pigo kubwa kutokana
na mvua hiyo iliyonyesha mwishoni mwa wiki kutokana na migomba mingi
kuanguka hivyo kutishia tishio la njaa.
"Siwezi kuelezea kwa undani tathmini ya
athari ya mvua hii lakini tumepata pigo kwani kaya nyingi migomba
imeangushwa na mvua hiyo" alisema Mwangosi.
Mkazi mwingine wa kijiji hicho Julius Mwambola alisema mvua hiyo imeangusha migomba yake 100 yenye thamani ya sh.250,000.
"Tumeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua
hii kwani mimi binafsi migomba iliyoangushwa na upepo wa mvua hiyo ni
zaidi ya 100" alisema Mwambola.
Mkazi mwingine wa Kijiji cha Mpuguso
kitongoji cha Nkuju, Tulinagwe Naswila alisema mvua hiyo imeangusha
migomba yake 40 yenye thamani ya sh.200,000.
Alisema mvua hiyo ilianza kunyesha saa
saba mchana na ilidumu kwa muda wa saa moja na kuleta athari kubwa ya
kubomoa baadhi ya nyumba na kuharibu migomba.
"Mvua ilikuwa kubwa ambayoiliharibu
migomba na kuezua paa za nyumba kadhaa na kubomoa nyumba ya mjane mmoja
aliyemtaja kwa jina la Gwanaloli Ndapapa (85).
Jitihada za kumpata Mkuu wa Wilaya ya
Rungwe, Julius Chalya ili kuzungumzia suala hilo zilishindikana baada ya
kupigiwa simu mara kadhaa bila ya kupokelewa.
0 comments:
Post a Comment