NAIBU WAZIRI MASAUNI AIONGOZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA KUTEMBELEA GEREZA LA KILIMO SONNGWE
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akijibu maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari baada ya kumaliza
ziara ya kutembelea shamba la Mahindi linalomilikiwa na Gereza la Kilimo
Songwe, lililopo wilayani Mbalizi, jijini Mbeya.(Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi)
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally, akiwaongoza wajumbe wengine wa
kamati hiyo kusalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza wakati wa ziara
ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Gereza la
Kilimo Songwe, wilayani Mbalizi, Jijini Mbeya.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(wapili kulia), akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally
(wakwanza kulia), kuingia ndani ya Gereza la Kilimo la Songwe,lililopo
wilayani Mbalizi, jijini Mbeya, ambapo wajumbe wa kamati walipata fursa
ya kusikiliza maoni kupitia risala iliyoandaliwa na wafungwa wa gereza
hilo.Wengine ni viongozi wa gereza hilo.
Afisa
wa Jeshi la Magereza akijibu maswali yaliyoulizwa na wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
walipotembelea shamba la mahindi linalomilikiwa na Gereza la Kilimo la
Songwe, lililopo wilayani Mbalizi, mkoani Mbeya.Wa kwanza kulia ni Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akimpokea Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally (wa pili kushoto),
wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa
na Gereza la Kilimo Songwe, wilayani Mbalizi, mkoani Mbeya.
(IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)
0 comments:
Post a Comment