Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta pamoja na viongozi wa mataifa mabalimbali wakiwa katika picha ya
pamoja katika jengo jipya la kituo cha Amani na Usalama (JULIUS NYERERE) lililopo
katika Makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa nchini Ethiopia.(PICHA NA IKULU)
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Viongozi Wakuu wa
Mataifa mbalimbali hawapo (pichani) katika Jengo jipya la Kituo cha Amani na
Usalama kilichopewa jina Rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini
Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati
wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya Umoja wa Afrika
kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis
Abba nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius
Nyerere katika kituo hicho cha Amani na Usalama.
0 comments:
Post a Comment