Mratibu wa Mafunzo
ya Mabingwa wa Tiba ya Mifupa nchini (SICOT , Société
Internationale de Chirurgie Orthopédique et de Traumatologie) Dk. Robert Mhina (kulia) kutoka Taasisi ya Mifupa
Tanzania (MOI) , akishiriki mafunzo ya utoaji huduma kwa majeruhiwa wa ajali
kwa njia ya video yaliyoratibiwa na kufanyika kwa njia ya video kwenye kumbi za
Wakala ya Mafunzoa kwa Njia ya Mtandao, yakijumuisha nchi. Kushoto ni
Dk.Lukwinyo na Dk.Mbaruku Mlinga.
Madaktari mbalimbali wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini.
Madaktari wa Tiba
ya Mifupa wakishiriki mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Dk.Hamid Masoud,
Dk.Valentine Restus na Dk. Joseph Msemwa.
Na Dotto Mwaibale
UMOJA wa Madaktari Bingwa wa Mifupa
Duniani (SICOT) ikishirikiana na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao
(TaGLA), umetoa elimu ya kutoa huduma kwa majeruhi wa ajali kwa njia ya
mtandao wa mafunzo kwa njia ya video.
Umoja huo ulitoa elimu hiyo kwa
kushirikiana na Madaktari Bingwa na wataalamu wa Mifupa kutoka nchi za
Tanzania, Marekani, Pakistani na Brazil.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo
akiwa TaGLA, Dar es Salaam, Mratibu wa Umoja huo hapa nchini, Dk. Robert
Mhina alisema kupitia mafunzo haya wameweza kujadili mambo mbalimbali
yahusuyo ajali za barabarani.
“Huwa tunajadili mada mbalimbali kama
ajali za barabarani kwa kubadilishana uzoefu na Madaktari wa nchi
nyingine kwa kutumia mtandao wa mafunzo kwa njia ya video, na wakati
wote huwa tunazungumza na nchi kutoka mabara mengine ili kubadilishana
uzoefu,”alisema.
Alisema madaktari hao huwa wanakubaliana
katika kujadili mada na kujadili kuhusu mambo muhimu yanayohusu tiba ya
mifupa huku wakipeana majukumu.
“Kupitia vikao hivi hutusaidia sana hata
kwa wale wanafunzi wanaojifunza Ubingwa kuona kitu gani kinaendelea
duniani, bila gharama za kusafiri nje ya nchi” alisema Dk Mhina.
Alisema tayari Umoja huu inaangalia
uwezekano wa kutoa nafasi kwa wanafunzi kutembela vituo kingine katika
nchi hizo ili kuona na kuongeza uzoefu zaidi.
“Mwaka huu kuna vikao kama sita hivi,
kikao hiki ni mwazo tu,”alisema na kuongeza kuwa kupitia mkutano huo
itawasaidia wananchi kwa kuboreshewa ufanyaji wa tiba sahihi za mifupa
hivyo kupata huduma za matibabu zilizoboreshwa kutokana na ajali za
barabarani.
Watoa mada katika mkutano huo
uliofanyika kwa njia ya video walikuwa ni pamoja na Dk. Syed M. Avais wa
King Edward Medical University, Dk. Robert D. Zura wa Louisiana State
University Health Science Center na Dk. Robert I. Mhina, wa Taasisi ya
Mifupa Tanzania (MOI) kutoka nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment