Saturday, November 11, 2017

frank Mvungi- Maelezo , Dodoma
 Serikali Kuendelea Kuimarisha Matibabu ya Saratani nchini. Serikali imesema itaendelea Kupanua wigo wa Upatikanaji wa huduma za Matibabu kwa wagonjwa wenye saratani ili Kupunguza msongamano katika Hosipitali ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam. Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Leah Komanya Bungeni kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto , Waziri wa Mali Asili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala amesema kuwa Serikali inakamilisha maandalizi ya kuanzisha matibabu ya Saratani kwa kutumia mionzi katika Hosipitali ya Bugando Jijini Mwanza. Baadhi ya majengo kwa ajili ya huduma husika yamekamilika yakiwemo jengo ambalo ni maalumu kwa ajili ya kudhibiti mionzi ambapo ukuta wake umejengwa kwa zege nene la mita moja,jengo la kutolea huduma za mionzi, baadhi ya wataalamu wapo na baadhi ya mashine za matibabu kwa mionzi zimeshanunuliwa zikiwemo Cobalt 60 na CT Simulator. “Takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2009-2017 Hosipitali imetoa matibabu kwa wagonjwa 39,300 kati yao 12,200 wakiwa ni wapya sawa na wastani wa wagonjwa wapya 1500 kwa mwaka” Alisisitiza Dkt. Kigwangala. Akifafanua Mhe. Kigwangala amesema vifaa vingine ikiwemo brachytherapy na immobilization devices zinatarajiwa kuwasili mwezi Disemba mwaka huu. Aidha, kwa sasa huduma za Tiba ya Saratani zinazopatikana katika Hosipitali ya Bugando ni zile za matibabu yasiyo ya mionzi (chemotherapy) ambazo zilianza januari 2009 kufuatia Sera ya Serikali kutoa huduma hizo Kikanda. Kutokana na msongamano wa Wagonjwa wanaosumbuliwa na Ugonjwa wa Saratani uliopo katika Hospitali ya Ocean Road pamoja na gharama kwa ndugu wa wagonjwa, Serikali imeadhamiria kuboresha huduma za Afya kwa kupanua huduma hizo hadi ngazi ya Kanda. MAELEZO TV
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu