Saturday, February 24, 2018

 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia akitoa ufafanuzi
kwa waandishi wa habari kuhusu hali ya kifedha kwa shirikisho hilo na matarajio
baada ya FIFA kuwapa maelekezo ya kufuatilia fedha ambazo hawakuingiziwa
kutokana na matatizo ya viongozi waliyopita leo jijini Dar es Salaam.
:Waziri Wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu mambo mbalimbali
serikali iliyozungumza na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani Gianni
Infantino na Rais wa CAF Ahmad Ahamad alipokuwa nchini kwa ajili ya mkutanon wao leo jijini Dar es salaam 

 • FIFA kuongeza fedha za Maendeleo na Kujiendesha kwa Shirikisho

  Na Anitha Jonas –WHUSM

  24/02/2018
  Dar es Salaam.
  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuendeleza viwanja tisa nchini kufuatia
  kuongezeka kwa dau la pesa za Maendeleo na Kujiendesha zinazotolewa na
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA kuanzia mwaka 2019 .
  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
  na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari
  kuhusu mambo mbalimbali serikali iliyojadili na Rais wa FIFA Gianni Infantino
  alipokuwa nchini kwa mkutano wake hivi karibuni.
  ‘’Rais wa FIFA alieleza kuongeza mara nne ya kiwango cha pesa za maendeleo na
  kujiendesha walizokuwa wanatoa kwa mashirikisho kama TFF mpaka kufikia Dola
  Milioni Moja na Laki Mbili na Nusu kwa mwaka na kusema pesa hizo ndiyo zitumike
  kuendeleza viwanja vya michezo kwani uwepo wa viwanja ndio unaosaidia kukuza
  vipaji vya soka,’alisema Dkt.Mwakyembe.
  Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Waziri
  Mwakyembe alisisitiza kuwa Rais huyo wa FIFA ametoa msisitizo wa kutokuwa na
  huruma kwa kiongozi yoyote wa shirikisho atakayekuwa na matumizi mabaya ya
  pesa pamoja na kufanya udanganyifu kwani yeye yuko mstari wa mbele kupinga
  ufisadi katika sekta ya maendeleo ya Soka duniani.
  Pamoja na hayo nae Rais wa TFF Bw. Wallace Karia alitoa ufafanuzi wa hali ya
  kifedha kwa shirikisho na kueleza kufuatia kuwepo na matatizo katika shirikisho
  hilo FIFA ilikuwa imesitisha kuwapatia fedha hizo za maendeleo na kujiendesha
  tangu mwaka 2015 lakini baada ya kuingia uongozi mpya ambao FIFA wameridhika
  nao na wameshaupa utaratibu wa kufuatilia fedha hizo.
  ‘’Rais wa FIFA alitueleza kuwa fedha hizo ziko salama nchini Zurich ni kwamba tu
  hazikuwa zimeruhusiwa kuingia nchini na kwa sasa tumeshaanza mchakato wa
  kufuatilia fedha hizo kwa kuzingatia maelekezo ya FIFA hivyo basi tutakapo pata
  fedha hizo Shirikisho litaendeleza baadhi ya miradi ambayo tumekwisha
  iandaa,’alisema Bw. Karia.
  Pamoja na hayo rais huyo alitoa wito wa wakazi wa jiji la Tanga waliyovamia eneo
  linalotarajia kujengwa Technical Center ya mchezo wa soka basi waondoke mara
  moja kabla hawajachukuliwa hatua.
  ***************MWISHO********************
 
 wao leo jijini Dar es Salaam    

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu