Wednesday, March 21, 2018

ZIARA YA NAIBU WAZIRI SEKTA YA UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATASHASTA NDITIYE OFISI ZA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA VISIWANI ZANZIBAR

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, akisalimiana na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe (wa pili kushoto), alipowasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kwa ziara ya kikazi katika taasisi za Mawasiliano Zanzibar jana. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha TPC, Elia Madulesi.  
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha TPC, Elia Madulesi, akijitambulisha katika mkutano na Naibu Waziri wa Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, mjini Zanzibar, jana.  
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akijitambulisha kwa Naibu Waziri Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (kulia), mjini Zanzibar jana.
Meneja Ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Zanzibar, Esuvatie Masinga akimpatia Naibu Waziri Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (kushoto) taarifa kuhusu hali ya mawasiliano kisiwani Zanzibar katika ziara yake kisiwani humo jana. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Huduma Shirika la Simu Tanzania (TTCL) Makao Makuu, Husein Nguvu.
Meneja Mkazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Zanzibar, Mwanaisha Saidi akimpatia Naibu Waziri Atashasta Nditiye (kushoto), taarifa kuhusu shirika hilo, visiwani Zanzibar.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akimkaribisha  Naibu Waziri Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (kulia), kuzungumza na wafanyakazi wa taasisi za Mawasiliano visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (katikati), akizungumza na wafanyakazi wa taasisi za Mawasiliano visiwani Zanzibar. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe na kulia ni Mkuu wa Idara ya Huduma Shirika la Simu Tanzania (TTCL) Makao Makuu, Husein Nguvu.  
Baadhi ya wafanyakazi wa taasisi za Mawasiliano na waandishi wa habari, wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (hayupo pichani), wakati akizungumza nao jana.  
Mkuu wa Idara ya Huduma, Shirika la Simu Tanzania (TTCL) Makao Makuu, Husein Nguvu (kulia), akijibu moja ya maswali yaliyokuwa yameulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano. 
Naibu Waziri Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Msaidizi wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Zanzibar, Mohamed Ali Haji (kyulia), wakati akipatiwa maelezo kuhusu mfumo wa njia za mawasiliano kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar, wakati wa ziara yake katika taasisi za Mawasiliano visiwani humo jana.   
Naibu Waziri Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (kushoto), akimsikiliza mmoja wa wateja waliofika kupata huduma za mawasiliano katika Ofisi za TTCL, Zanzibar. Katikati ni  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe. 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akimpatia maelezo Naibu Waziri Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (wa pili kushoto), kuhusu moja ya mitambo ya ukaguzi wa mizigo na vifurushi, wakati wa ziara hiyo.
Naibu Waziri Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye (katikati), akioneshwa jinsi mashine ya ukaguzi (Scanner), inavyofanya kazi na mtaalamu wa mashine hiyo, Khalfani Mkahirika katika kukagua mizigo na vifurushi, vinavyosafirishwa na Shirika la Posta ndani na nje ya nchini visiwani humo jana.
Mkuu wa Kitengo cha EMS, Zanzibar, Mashavu Mmanga,  akimpatia maelezo Naibu Waziri Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, wakati wa ziara hiyo.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu