2


SI LA KULIKOSA

Tuesday, April 24, 2018

VICENT MBILINYI AJINOWA KUMKABILI HUSSEIN SHEMDOE MEI MOSI TANDIKA

0 commentsKocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimnowa bondia vicent Mbilinyi kwa kumuelekeza kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'Upcat' Mbilinyi anajiandaa na mpambano wake na Hussein Shemdoe utakaofanyika katika ukumbi wa musoma Bar siku ya Mei Mosi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu

BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea na mazoezi ya kumkabili Hussein Shemdoe wakati wa mpambano wao utakaofanyika mei mosi siku ya sikukuu ya wafanyaklazi Dunian mpambano uho utafanyika katika ukumbi wa Musoma Bar uliopo Tandika Mwembe Yanga mpambano wa raundi 8

Mbilinyi anaenolewa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amekuwa nje ya ulingo kwa mda wa mwaka mzima sasa tangu mwishoni mwa mwaka 2016 na sasa anakuja kivingine

mbali na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia mbali mbali ambapo bondia Shafii Ramadhani atapambana na Antony Mathias wakati Nassibu Ramadhani atavaana na Hamisi Mohamedi na Shomari Galibu atapambana na Hashimu Sheni wakati Said Mlugulu atavaana na Said Bakari 'Kidedea' 

Mapambano haya yoteyatafanyika siku hiyo katika ulingo mpya  wa mdau wa masumbwi nchini Zahoro Maganga 'Super Diego' aliejenga ulingo uho kwa ajili ya kuwakombowa mabondia na hadha ya kupigania chini 

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
-- 

Endelea Kusoma >>

TCRA YASISITIZA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA MITANDO NCHINI

0 comments
Katika kupambana na makosa ya uhalifu wa kimtandao nchini TCRA kwa kushirikiana na kampuni ya Kingdom Heritage ilifanya semina kwa vijana yenye lengo la kuwajengea uelewa wa namna nzuri ya matumizi na usalama Mtandao.

Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwaka wiki iliyopita katika ukumbi wa Buni Hub tume ya Sayansi Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na vijana kutoka vyuo na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.

Mwanansheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe alipokuwa akizungumza katika warsha hiyo alisema  kulingana na ukuaji wa miundombinu ya TEHAMA inakuwa kwa kasi na kusababisha matokeo chanya na hasi katika jamii zetu
“Katika majira haya ya maendeleo ya TEHAMA waharifu wanatumia mwanya huo kufanya uharifu katika mifumo mbali mbalimbali ya Kompyuta hivyo tunatakakiwa kuwa makini kwa watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA nchini,” alisema Dk Filikunjombe.

Alisema kama TCRA wanazidi kusisitiza kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao tena yenye maadili ili kupunguza uhalifu huo, Kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo cha uhalifu wa kimtandao.

Mwanzilishi wa Jamii Forums na muwasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo alizungumzia fursa mbalimbali zinazopatikana katika mitandao na miundombinu ya TEHAMA kwa kuwasihi vijana waliokuwa hapo kuwa wabunifu katika majira haya na kuja na mifumo suluhisho itakayoweza kutumika katika jamii zetu.

“Serikali pia kupitia wizara au mamlaka zinazohusika kusapoti juhudi za vijana wabunifu katika TEHAMA  kwa miundombinu na kanuni na taratibu rafiki ili waweze kujifanikisha katika ubunifu wao mpaka kijipatia kipato binafsi na tafa zima kwa ujumla.” Alisema Melo.

Mtaalamu wa masuala ya ulinzi katika mfumo ya Kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik, Robert Matafu alizungumzia  namna ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kimtandao na kuwa salama mtandaoni.

“Nchi nyingi za Afrika tunakosa uelewa wa maarifa ya kujilinda na mashambulizi ya kimtandao na kupelekea kupata hasara sana katika taasisi au watu binafsi kutokana na mashambulizi hayo,” alisema Matafu.

Aliongeza “Takwimu zinaonyesha taasisi nyingi afrika na Tanzania tukiwepo hatuwekezi vya kutosha katika mifumo ya kiulinzi na usalama mtandao,kwa kufanya hivyo tunaongeza asilimia kubwa za kupata mashambulizi ya kimtandao katika tasisi zetu,” alisema.

Awali, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage waandaaji wa semina hiyo Tunu  Bashemela alisema wao kwa sehemu yao wanaunga mkono juhudi za serikali kupitia TCRA katika kupambana na makosa ya uharifu wa kimtandao kwa kutoa elimu kwa umma hasa vijana ambao ndio rika linalotumia sana mitandao.

“Ili kujua matumizi sahihi na salama vijana mliopo hapa lazima mtambue kuwa sheria ya makosa ya uhalifu wa kimtandao ipo na inafanya kazi lazima tuheshimu na kutii vitu inavyotuzuia kufanya bali tutumie mitandao kwa namna za ubunifu zenye kutuletea fedha na kujiingizia kipato,” alisema Bashemela.Mwanansheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe

Mwanzilishi wa Jamii Forums mmoja kati ya wawasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage ambao ndio waandaaji wa semina hiyo Tunu  Bashemela
Vijana na mbalimbali watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA walioudhulia semina hiyo wakifuatilia kwa makiniMtaalamu na Mshauri wa masuala ya ulinzi katika mfumo ya kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik, Robert Matafu katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.
  Mtendaji Mkuu wa tzNIC  Abibu Ntahigiye katika mjadala wa katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.
Mwanzilishi wa Jamii Forums katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.
Story Katika kupambana na makosa ya uhalifu wa kimtandao nchini TCRA kwa kushirikiana na kampuni ya Kingdom Heritage ilifanya semina kwa vijana yenye lengo la kuwajengea uelewa wa namna nzuri ya matumizi na usalama Mtandao. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwaka wiki iliyopita katika ukumbi wa Buni Hub tume ya Sayansi Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na vijana kutoka vyuo na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi. Mwanansheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe alipokuwa akizungumza katika warsha hiyo alisema kulingana na ukuaji wa miundombinu ya TEHAMA inakuwa kwa kasi na kusababisha matokeo chanya na hasi katika jamii zetu “Katika majira haya ya maendeleo ya TEHAMA waharifu wanatumia mwanya huo kufanya uharifu katika mifumo mbali mbalimbali ya Kompyuta hivyo tunatakakiwa kuwa makini kwa watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA nchini,” alisema Dk Filikunjombe. Alisema kama TCRA wanazidi kusisitiza kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao tena yenye maadili ili kupunguza uhalifu huo, Kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo cha uhalifu wa kimtandao. Mwanzilishi wa Jamii Forums na muwasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo alizungumzia fursa mbalimbali zinazopatikana katika mitandao na miundombinu ya TEHAMA kwa kuwasihi vijana waliokuwa hapo kuwa wabunifu katika majira haya na kuja na mifumo suluhisho itakayoweza kutumika katika jamii zetu. “Serikali pia kupitia wizara au mamlaka zinazohusika kusapoti juhudi za vijana wabunifu katika TEHAMA kwa miundombinu na kanuni na taratibu rafiki ili waweze kujifanikisha katika ubunifu wao mpaka kijipatia kipato binafsi na tafa zima kwa ujumla.” Alisema Melo. Mtaalamu wa masuala ya ulinzi katika mfumo ya Kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik, Robert Matafu alizungumzia namna ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kimtandao na kuwa salama mtandaoni. “Nchi nyingi za Afrika tunakosa uelewa wa maarifa ya kujilinda na mashambulizi ya kimtandao na kupelekea kupata hasara sana katika taasisi au watu binafsi kutokana na mashambulizi hayo,” alisema Matafu. Aliongeza “Takwimu zinaonyesha taasisi nyingi afrika na Tanzania tukiwepo hatuwekezi vya kutosha katika mifumo ya kiulinzi na usalama mtandao,kwa kufanya hivyo tunaongeza asilimia kubwa za kupata mashambulizi ya kimtandao katika tasisi zetu,” alisema. Awali, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage waandaaji wa semina hiyo Tunu Bashemela alisema wao kwa sehemu yao wanaunga mkono juhudi za serikali kupitia TCRA katika kupambana na makosa ya uharifu wa kimtandao kwa kutoa elimu kwa umma hasa vijana ambao ndio rika linalotumia sana mitandao. “Ili kujua matumizi sahihi na salama vijana mliopo hapa lazima mtambue kuwa sheria ya makosa ya uhalifu wa kimtandao ipo na inafanya kazi lazima tuheshimu na kutii vitu inavyotuzuia kufanya bali tutumie mitandao kwa namna za ubunifu zenye kutuletea fedha na kujiingizia kipato,” alisema Bashemela.
Endelea Kusoma >>

WANAWAKE NI NGUZO YA MAENDELEO KATIKA KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA - DC MCHEMBE

0 comments
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe akipongezwa na mchungaji Canon Chamwenye wa kanisa Anglikana Msingisi mara baada ya kumaliza kuongea na akina mama juu ya kuanzisha kiwanda ili waweze kujikwamua katika maisha yao.
Mmoja ya akinamama akitoa shukrani ya kuku kwa mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe afanikisha ushawishi wa ujenzi wa viwanda kwa kuanzia na wanawake kanisa la Anglikana Dinari ya Rubeho Gairo. Ushawishi huo ulianza mwezi wa sita mwaka 2017 ambapo Mhe. Mchembe alihudhuria mkutano wa wanawake wa kanisa hilo akiwa Mgeni Rasmi. Katika mkutano huo Mhe. Mchembe aliwashawishi akinamama hao kupitia umoja wao waanzishe kiwanda ili kiwainue kiuchumi. Aidha wapate mahali pa kuuza mbegu za alizeti ambazo kwa sasa alizeti ni kati ya mazao makuu ya biashara wilayani Gairo. Hatimaye mpango umekamilika na Mhe. Mchembe amechangia pesa za Kitanzania shilingi laki tano kuhamasisha ujenzi wa kiwanda. Jumla ya gharama ya mradi ni shilingi milioni kumi na tisa. Majengo yanaendelea kufunguliwa na mradi unategemewa kuanza mwishoni mwa mwaka 2018. Mkuu wa Wilaya aliwashukuru wana Dinari hiyo iliyojumuisha Kata ya Rubeho na Msingisi. Wanawake ni nguzo ya Maendeleo katika uchumi wa viwanda. --
Endelea Kusoma >>

RAIS MAGUFULI AUFAGILIA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF KWA UWEKEZAJI WENYE TIJA DODOMA

0 comments
d
 Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mwenye mkasi), akiungana na baadhi ya mawaziri na viongozi wengine kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, (PSPF DODOMA PLAZA), mjini humo Aprili 23, 2018. Jengo hilo lenye urefu wa ghorofa 12, tayari limepangishwa kwa takriban asilimia 100.
 Rais Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mara baada ya kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitega uchumi la Mfuko huo mjini Dodoma.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Dodoma


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amefurahishwa na uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF wa kujenga jingo la kitegauchumi mkoani Dodoma.


Kilichomfanya Rais Magufuli kufurahishwa na uwekezaji huo ni kuona jengo hilo lenye ghorofa 12 tayari limepangishwa kwa asilimia 100 hata kabla ya uzinduzi rasmi uliofanyika Aprili 23, 2018.
“Ninyi mmemaliza tu tayari asilimia 100, mliangalia kwamba Dodoma ni makao makuu na mahitaji ya nahitajika kwa ajili ya majengo, hongereni sana kwa kupanga mikakati yenu vizuri kisayansi.” Alisema Dkt. Magufuli na kutoa hakikisho, “Pamoja na kuunganishwa kwa Mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii ninyi wafanyakazi wa PSPF mjihesabu kuwa hamtapoteza nafazi zenu, lakini pia jengo hili limeboresha na kupendezesha mandhari ya Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi yetu.” Alisema Rais Magufuli wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa jengo hilo uliokwenda sambamba na ufunguzi rasmi wa makao makuu ya NMB Bank (Kambarage) ambao ni miongoni mwa wapangaji wakubwa kwenye jingo hilo lililoko barabara ya kuelekea chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Rais pia alifurahishwa na ushiriki wa watanzania katika ujenzi wa jengo hilo.
“Nimefurahi kusikia kuwa jingo hili limesanifiwa na ujenzi wake kusanifiwa na watanzania, ma contractors na consultants na kwamba takriban watanzania 250 walipata ajira wakati wa ujenzi.” Alipongeza.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alisema, PSPF ndio Mfuko wa kwanza wa Hifadhi ya Jamii kuweka kitegauchumi cha jingo mkoani Dodoma na hivyo kuisaidia serikali ya awamu ya tano katika azma yake ya kuhamia makao makuu ya Nchi, mjini Dodoma.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu,
akielezea historia ya uwekezaji huo alisema, Mfuko ulipewa viwanja vya mradi huu na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) mwaka 2012 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuendeshea shughuli za Mfuko pindi inapotokea dharura (business continuity) pamoja na kibiashara. Kazi ya usanifu na ujenzi wa jengo hili lilianza Julai 2015 na kukamilika Januari 2018 na kwa sasa jengo liko kwenye kipindi cha uangalizi (Defect Liability Period) ambacho kitaisha Januari 2019. Gharama tarajiwa za mradi yaani “contract sum” ni shilingi bilioni 37.02. Mpaka sasa Mfuko umeshalipa kiasi cha Shilingi za Kitanzania bilioni 30.56.
Jengo hili lina minara miwili, mmoja ukiwa na ghorofa 11 na mwingine ukiwa na ghorofa 3. Ukubwa wa jengo ni mita za mraba 15,741.60 pamoja na eneo la maegesho kwa ajili ya magari 161. Matumizi ya jengo ni kwaajili ya ofisi na shughuli za kibiashara.
“Hadi sasa jengo limepata wapangaji ambao kwa uchache ni kama ifuatavyo; NMB Bank, AZANIA Bank, TIB Corporate Bank, Benki ya Kilimo, GIZ, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), TASAF, TANAPA, TBS, Gaming Board, PPRA, Makao Makuu ya TARURA, Wizara ya Mambo ya Ndani, Sekretarieti ya Maadili ya Watumishi wa Umma, Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambao hawa pamoja na wengine wanafanya jengo kuwa limepangishwa kwa asilimia 98. Na kufikia leo Mfuko umeshakusanya kiasi cha Shilingi za Kitanzania 1.06 bilioni kutokana na malipo ya  pango na tunatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 4.7 kwa mwaka na kufikia miaka minane mradi utakua umerejesha fedha zote zilizowekezwa.”Alibainisha Bw. Mayingu.

 Rais akitoa hotuba yake.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Mhandisi Musa Iyombe, akitoa hotuba yake.
 Bw. Mayingu akitoa hotuba yake.
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibese, (kulia), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, (wakwanza kushoto), na Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP), Simon Siro, wakati wa uzinduzi huo.
 Wakurugenzi wa PSPF
 Mameneja wa PSPF
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Binilith Mahenge, (kushoto), akipokewa na Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akiwasili kwenye eneo la tukio.
 Rais, baadhi ya mawaziri na viongozi wengine, wakiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya wadhamini na wafanyakazi wa PSPF.
 Hili ndio jingo la PSPF DODOMA PLAZA lenye ghorofa 12 lililozinduliwa na Rais John Magufuli mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akitoa hotuba yake.
 Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri, kutoka kushoto, Mhe. Luhaga Mpina (Waziri wa Mifugo na Uvuvi), Mhe.Juliana Shonza, (Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, (Waziri wa Elimu) na Mhe.Jumaa Aweso, (Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji).
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (kulia), akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mwishoni mwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa PSPF, Bi.Costantina Martin, (kushoto), akibadilishana mawazo na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abass, (katikati) na Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
Kikundi cha Sanaa kikitumbuiza kwenye hafla hiyo.
Endelea Kusoma >>

BILIONI 256 KUTUMIKA KUJENGA KIWANDA CHA KEMIKALI MLANDIZI

0 comments

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa tano kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa Nne kulia) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson (wa tatu kulia) na baadhi ya Viongozi wakifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kemikali cha Msufini (T) Ltd,  Mlandizi mkoa wa Pwani, leo. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Wakifurahia baada ya kuweka Jiwe la Msingi
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF, Regnald Mengi, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kemikali cha Msufini (T) Ltd,  Mlandizi mkoa wa Pwani, 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akihutubia kwa niaba ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kemikali cha Msufini (T) Ltd,  Mlandizi mkoa wa Pwani
****************************************************
SERIKALI imezindua mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kemikali za kutengeneza dawa za kusafishia maji kitakachogharimu sh. Bilioni 256.
Uzinduzi huo umefanyika eneo la Mlandizi  Msufini mkoani Pwani jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kwa niaba ya Makamu wa Rais, Samiah Suluhu Hassan.
Mwijage alisema mradi huo ukikamilika utasaidia serikali kuokoa kiasi cha  fedha kilochokuwa kikitumika kununua dawa hiyo nje za nchi.
" Mradi huo ni wa tatu kwa ukubwa Afrika   na kwa sasa tunatarajia kuzindua viwanda vingine tisa vilivyo na viwango. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Endelea Kusoma >>

Wednesday, April 11, 2018

0 comments

16 Millions to be Won

HEART MARATHON

29th April 2018 | 06:00am | COCO BEACH

REGISTER NOW www.heartmarathon.com

For Registration

+255 684 244 377 | +255 683 907 080
Email: info@heartmarathon.com | www.heartmarathon.com
***
123Tanzania E-Shots
123Tanzania.com is the largest B2B online directory of Tanzania with more than 40,000 monthly visitors
Contact 123tanzania.com: English or Kiswahili +255 786 110 021, +255 786 792 976, +255 22 213 3039
123Tanzania Ltd, Sabodo Car Parking Tower, 10th Floor, India Street, P. O. Box 8758, Dar es Salaam, Tanzania
Telephone: +255 22 213 3039 | Email: info@123tanzania.com | Web: www.123tanzania.com
You are receiving this email from 123tanzania.com, Tanzania's largest Business portal. If you would like to unsubscribe from this list, simply click unsubscribe from the link below
 
©2018 123Tanzania | Sabodo Car Park, 10th Floor, India Street, DSM

Endelea Kusoma >>
 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu