SERIKALI YAWATAKA WADAU WA NGOs KUENDELEA KUTEKELEZA SERA ZILIZO CHINI YA IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII
Na Mwandishi wetu Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeawataka wadau wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuendelea kutekeleza Sera mbalimbali zilizo chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii katika utekelezaji wa majukumu yao.
Hayo yamesemwa Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi na Msajili wa NGOs Bw. Marcel Katemba Jijini Dodoma wakati wa Kikao kati ya Serikali na Wadau hao kinachokaa kwa siku moja kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi zao na kutekeleza Sera zilizo chini Idara kuu Maendeleo Jamii.
Ameongeza kuwa katika kutekeleza Sera mbalimbali Serikali inashirikiana na Wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanafanya kazi kubwa nchini katika kuleta maendelo ya jamii na Taifa katika sekta mbalimbali nchini.
“Wadau wa NGOs mnafanya kazi nzuri na kubwa katika kuleta matokeo chanya kwa jamii na taifa letu” alisisitiza Bw.Katemba.
Kwa upande wake Mwakilishi Kutoka Shirika la World Vision Tanzania Bi. Janeth Edson akitoa mrejesho wa makubaliano kati ya Serikali na NGOs kwa upande wa NGOs amesema kuwa wao kama wadau wataendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Sera mbalimbali na kuwaasa wadau kuendelea kuunganisha nguvu na Serikali katika kusogeza mbele gurudumu la maendeleo.
MWISHO.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi akitoa mrejesho wa maendeleo ya utekelezaji wa hati ya makubaliano na ushirikiano kati ya wadau wa NGOs baina ya Serikali na NGOs kwa upande wa Serikali katika kikao kati ya Serikali na wadau hao Jijini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment