Wednesday, December 26, 2012

Padiri apigwa risasi Zanziba

Padiri apigwa risasi Zanziba


 Photos by Martin Kabemba
Ni harakati za kumsafirisha Padri Ambrose Mkenda wa kanisa la Katolik la Mpendae zanzibar kwenda Dar es Salaam kupata matibabu zaidi baada ya kupigwa risasi na watu ambao hadi jana mchana hawajakamatwa



Padiri apigwa risasi Zanziba


SIKU chache tu baada ya Katibu wa Mufti Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga, kumwagiwa tindikali, kiongozi mwengine wa dini amepigwa risasi huko Zanzibar na watu wasiyojulikana.

Padiri Ambrose  Mkenda wa Kanisa la Romani katoliki alipigwa risasi nyumbani kwake  Tomondo saa 1:45 wakati wa sikukuu ya Krismasi katiika tukio ambalo polisi tayari wamelihusisha na ujambazi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Azizi Juma Mohamed alisema jana mjini hapa kuwa Padiri alipigwa risasi katikati ya kidevu na taya wakati anasubiri kufunguliwa geti nyumbani kwake aikiwa ndani ya gari yenye usajili Z 586 AW aina ya Toyota Rav4.

Alisema kwamba Padiri Mkenda alikuwa anatoka kumwangalia Padiri mwezake Peter Minja ambaye amelazwa katika hospitali ya mnazi mmoja.

 Hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Akizungumzia zaidi tukio hilo Kamanda Azizi  alisema Padiri Mkenda alipigwa risasi mbili ambazo maganda yake polisi wamefanikiwa kuyapata katika eneo la tukio.

Alisema kwamba watu waliompiga risasi walikuwa na silaha aina ya bastola na Kiongozi huyo alipigwa kwa umbali wa mita mbili.

Kamanda huyo alisema baada ya mlinzi kutoka nje alikuta kiongozi huyo tayari ameopigwa risasi na watu hao wakiwa wametoweka
Padiri apigwa risasi Zanziba
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu