MKUU WA MAJESHI GENERALI DAVIS MWAMUNYANGE AKISUBIRI KUPOKEA MIILI YA VIJANA WAKE WALIOUAWA SUDAN |
BAADHI YA VIONGOZI WA SERIKALI WAKIONGOZWA NA MAKAMU WA RAIS DR MOHAMMED GHARIB BILAL |
MAMA SALMA KIKWETE NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM NAO WALIKUWEPO |
NDEGE ILIYOBEBA MIILI YA WANAJESHI MARA BAADA YA KUWASILI KUTOKA SUDAN |
MIILI YA WANAJESHI 7 WALIOUAWA SUDAN IKIONEKANA KWENYE NDEGE MARA BAADA YA KUWASILI |
WANAJESHI WA JWTZ WAKIBEBA MIILI YA WENZAO WALIOUAWA HUKO SUDAN |
NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WAKISUBIRI KUWASILI KWA MIILI YA WANAJESHI WALIOUAWA SUDAN |
ILIKUWA NI VIGUMU KUVUMILIA HALI HII BAADA YA KUONA MIILI YA WAPENDWA WAO |
HALI ILIKUWA YA MACHUNGU KWA NDUGU WA KARIBU |
WANAJESHI WA JWTZ WAKIPOKEA MIILI YA WENZAO |
MIILI IKITOLEWA KWENYE NDEGE |
MMOJA KATI YA MIILI YA MAREHEMU UKIINGIZWA KWENYE GARI |
MOJA KATI YA FAMILIA ZA MAREHEM WALIOUAWA SUDAN |
FAMILIA ZA MAREHEM WAKISUBIRI KUWAPOKEA WAPENDWA WAO |
Kaimu Mkurugenzi wa habari wa JWTZ, Meja Joseph Masanja amesema miili hiyo imewasili leo Jumamosi majira ya saa 9.45 alasiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNIA na imehifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo hadi Julai 22 ambapo itaagwa rasmi.
Miili iliyowasili ni ya Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte. Fortunatus Msofe.
Shughuli za kuagwa miili ya wanajeshi hao zitafanyika katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa vilivyoko Upanga jijini Dar es salaam.
Kuwapoteza wanajeshi hawa ni la kwanza na kubwa kwa nchi ya Tanzania tangu Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007. Wanajeshi wengine watatu wa Tanzania walifariki dunia mwezi uliopita baada ya chombo chao cha kusafiria kusombwa na maji ya mto uliokuwa umefurika huko nchini Sudan.
HABARI/PICHA NA BONGOCLAN.COM
0 comments:
Post a Comment