MH MAGUFULI NA MGOMBEA MWENZA WAKE, SAMIA SULUHU HASSAN WATAMBULISHWA ZANZIBAR
Mgombea Urais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alipozungumza na
Wananchi na wanachama wa CCM Mkoawa Mjini leo katika mkutano wa
kutambulishwa uliofanyika leo katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM
Kisiwandui Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Mgombea
Urais wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea mwenza
Mhe,Samia Suluhu Hassan (kushoto) wakiwa Makamo wa Pili wa Rais wa
zanzibar na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafya Silima Juma (kulia)
kwa pamoja wakimuombea dua Marehemu Mzee Abeid Amani Karume katika
Kaburi lake Ofisi ya CCM Kisiwandui leo kabla ya kutambulishwa kwa
Wananchi wa Zanzibar baada ya uteuzi wao uliofanyika Dodoma hivi
karibuni,[Picha na Ikulu.]
Mgombea Urais wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli (CCM) akisalimiana na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipowasili
viwanja vya CCM Kisiwandui katika mkutano wa kutambulishwa rasmi akiwa
na mgombea mwenza Mhe,Samia Suluhu Hassan leo,[Picha na Ikulu.]
Mgombea
Urais wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli akifuatana na Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (katikati) pamoja na Mgombea Mwenza
Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafya
Silima Juma baada ya wagombea hao kuvalishwa Skafu na Vijana Chikpukizi
walipofika katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
palipofanyika Mkutano wa kutambulishwa rasmi kwa Wananchi leo,[Picha na
Ikulu.]
Mgombea
Urais wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea mwenza
Mhe,Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wazee wa CCM mara walipowasili
katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja wakatti wa
Mkutano wa kutambulishwa rasmi kwa Wananchi leo,[Picha na Ikulu.]
Wananchi
na wanaCCM wa Mkoa wa Mjini waliofika katika mkutano wa kutambulishwa
Mgombea Urais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Mgombea mwenza
Mhe,Samia Suluhu Hassan wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgombea huyo
wakati alipozungumza nao leo katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM
Kisiwandui Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mgombea
mwenza wa Urais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan(kulia)Picha na
Ikulu.] Kwa hisani ya ZanziNews
You might also like:
0 comments:
Post a Comment