Na:
Lilian Lundo - MAELEZO
15/08/2016
Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeeleza kuwa ifikapo Desemba 31 mwaka huu jumla
ya watanzania milioni 23 watakuwa na namba za utambulisho wa vitambulisho vya Uraia.
Kaimu Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Rose Mdami amesema kuwa hatua hiyo ni utekelezaji
wa agizo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli la kuitaka Mamlaka hiyo kuweka saini ya
mwombaji na mtoaji wa vitambulisho hivyo.
“Tumeanza kutekeleza
agizo la Mhe. Rais tangu mwezi Juni mwaka huu, hii inamaanisha kwamba vitambulisho
vyote tulivyochapisha kuanzia mwezi Juni mpaka leo vina saini ya muombaji,
saini ya mtoaji na tarehe ya kuzaliwa muombaji” amefafanua Mdami.
Ameeleza kuwa kazi ya
ugawaji wa vitambulisho hivyo inasubiri kuzinduliwa na Mhe. Rais Dkt. John
Pombe Magufuli atakayekabidhiwa kitambulisho
cha uraia namba moja na baadaye vitambulisho hivyo kugawiwa kwa wananchi wengine.
Mdami amesema ifikapo
Desemba 31 mwaka huu NIDA itakuwa imetoa namba za utambulisho wa vitambulisho hivyo
kwa watanzania milioni 23 kwa kutumia
taarifa za Tume ya Uchaguzi (NEC) zilizo katika vitambulisho vya kupigia kura na kuzihamishia katika kanzi data ya NIDA.
Amefafanua kuwa ili mwananchi aweze kupata kitambulisho
cha uraia atalazimika kufika katika ofisi za NIDA akiwa na vielelezo
vinavyoonyesha mwaka wake wa kuzaliwa pamoja udhibitisho wa uraia wake hii ni
kutokana na NEC kutokuwa na viambatanisho hivyo.
Amebainisha kuwa mwananchi
mwenye namba ya utambulisho anaweza kupata huduma zote zinazohitaji namba ya
kitambulisho cha Uraia kutokana na namba hiyo kutobadirika na kuendelea
kutumika hata baada ya kitambulisho kuchapishwa.
Amesema mpaka sasa watanzania
milioni 2.7 wamekwisha patiwa vitambulisho
hivyo na milioni 6.5 wamesajiriwa kwa ajili ya kupata vitambulisho
hivyo.
Aidha, Vitambulisho
hivyo vya zamani vitaendelea kutumika mpaka utakapotangazwa utaratibu wa
kuvibadirisha kwa ajili ya kupata vitambulisho vipya.
Pia ametoa ufafanuzi
juu ya malalamiko ya baadhi ya watu wanaodai kwamba wa kumekuwa na mlolongo mrefu
wa kupata vitambulisho hivyo kwa kueleza kuwa NIDA haina namna ya kufupisha
mlolongo huo kwani kufanya hivyo ni sawa na kuuza uraia wa Tanzania.
Amesisitiza kuwa ni lazima NIDA ijiridhishe
juu ya uhalali na sifa za muombaji ni kuwa ni Mtanzania kwa kuambatanisha
vielelezo vinavyohitajika.
MWISHO
![]() | ||||
|
0 comments:
Post a Comment