Na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imetakiwa kuendelea kuwaandaa
wataalamu katika fani za Elimu ya Watu Wazima na Maendeleo ya Jamii wenye
ubunifu wa kutatua changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Stadi za Kusoma,
Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa vijana na watu wazima.
Akizungumza wakati wa mahafali ya 53 ya Taasisi hiyo jijini Dar es
Salaam leo, Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Tate Ole
Nasha amesema ili kudhibiti ubora wa elimu inayotolewa kuna umuhimu
wa kuwa na Sheria ya Elimu ya Watu Wazima itakayotoa mamlaka kwa Taasisi kuweza
kusajili na kuthibiti ubora wa Vituo vya Elimu nje ya mfumo rasmi.
Akieleza mikakati ya Serikali kuboresha elimu hapa nchini Mhe.
Ole Nasha amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano mara tu baada ya kuingia
madarakani ilianza utekelezaji wa Mpango wa Elimu bila malipo ambapo
kiasi cha shilingi bilioni 23 hutumika kila mwezi katika
mpango huo.
Aidha mhe. Ole Nasha alitoa wito kwa wazazi kuendelea
kuwaandikisha shule watoto wote waliofikisha umri wa kujiunga na shule ili
waendane na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza uwajibikaji katika
kuchochea maendeleo ya Taifa.
Akizungumzia
swala la kukuza elimu nchini Ole nasha amesema kuwa kwa mujibu wa Sensa ya Watu
na Makazi ya mwaka 2012, idadi ya Watanzania wasiojua Kusoma, Kuandika na
Kuhesabu (KKK) ni asilimia 22 ambapo asilimia hii bado ni kubwa na ni changamoto katika kufikia azma ya kuwa na Watanzania walioelimika na wanaoweza kuchangia kwa haraka katika
maendeleo ya Taifa letu kama
inavyobainishwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.
“Naipongeza Taasisi
ya Elimu ya Watu Wazima kwa kazi nzuri katika kuwaandaa wataalamu na
Uwajibikaji wenu ndio umewezesha kuwapata wahitimu hawa 962 ambao
naamini wameandaliwa vizuri na wameiva katika taaluma zao, hivyo watashiriki
kikamilifu katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi” Alisisitiza
Mhe. Ole Nasha
Akifafanua Mhe. Ole Nasha amesema kuwa wahitimu hao hawana budi
kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya
Tano Mhe. Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli
ya HAPA KAZI TU kwa vitendo.
Mahafali ya 53 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima yameshirikisha
wahitimu wa Astashahada, Stashahada na Shahada na yamefanyika katika Viwanja
vya Taasisi hiyo ambapo Dhamira ya
Serikali Awamu ya Tano ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kuibadili Tanzania
kuwa nchi ya uchumi wa kati inayotegemea viwanda ifikapo 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumzia mikakati ya Taasisi hiyo katika kukuza kiwango cha elimu nchini wakati wa mahafali ya 53 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
PIX3. Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.
Tate Ole Nasha akimtunuku cheti cha uongozi bora kiongozi wa Serikali ya
Wanafunzi TEWW, Thomas Amos wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika katika
Viwanja vya Taasisi hiyo Jijini Dar es
Salaaam.
.Baadhi ya Wahitimu wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati
wa mahafali hayo
0 comments:
Post a Comment