DK NDUGULILE AZINDUA PROGRAMU YA KIKUNDI MLEZI KWA WANAWAKE WAJASILIAMALI.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akinunua mvinjo kwa moja ya kikundi cha wanawake wajasiliamali Wilayani Kisarawe ikiwa ni kuunga mkono uzaendo wa kununua bidhaa kutoka kwa wazawa wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akingalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha wanawake wajasiliamali cha Tutashinda Wilayani Kisarawe wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani Pwani.
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amezindua programu ya Kikundi Mlezi
yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasilimali wasio katika Sekta rasmi kuleana wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza mitaji na biashara zao.
Dkt. Ndugulile amezindua programu hiyo wakati
alipofanya ziara Wilayani Kisarawe mkoani Pwani katika zoezi la kuamsha ari ya
wananchi kujishughulisha katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Dkt.Ndugulile amesema kuwa ili kufanikisha kufikia Tanzania ya viwanda
Serikali itaendelea kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo hasa wanawake katika
kuwawezesha kuanzisha vikundi vitakayoanzisha viwanda vidogo vidogo na vya
kati.
Ameongeza
kuwa lengo la kuzindua Programu ya
Kikundi Mlezi ni inalenga kuwawezesha wanawake wasio katika Sekta rasmi
kwa kuwashirikisha wanawake wajasilimali waliokomaa katika
biashara kuwalea na kuwasaidia wanawake wajasiliamali wanaoanza shughuli
hizo.
“Niseme programu hii itasaidia kwa asilimia kubwa
kuibua wanawake ambao hawakuwa na uwezo katika kuanzisha biashara zao na
kufanya wanawake kujiunga na vikundi kukuza biashara na miradi yao na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na
vya kati”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Bibi.Sihaba Nkinga amesema kuwa programu ya Kikundi Mlezi
itasaidia kuwainua wanawake na kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli
za uzalishaji.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kisarawe Bw. Musa Gama amesema kuwa ataendelea kushirikiana na Wizara
kuhamasisha wanawake kujitokeza na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika
kuendesha biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Mmoja
wa wanawake wajasiliamali Wilayani Kisarawe
Bi. Lydia Jacob ameishukuru Serikali kwa kuzindua Mpango huo
utakaowawezesha wanawake kuleana na kusaidiana katika kuanzisha na
kuinuka
katika biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amefanya ziara ya siku moja mkoani
Pwani na kuwatembelea wanawake wajasiliamali katika kuhamasisha wanawake
kujishughulisha ili kusaidia kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwa
na Tanzania ya Viwanda.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment