JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA,
MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
|
Simu Na.255-26-2963341/2963342/2963346
Nukushi: 255-26-2963348
Nukushi: 255-26-2963348
Barua Pepe: ps@communitydevelopment.go.tz
Tovuti:www.mcdgc.go.tz
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU
USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 62 WA HALI YA MAENDELEO YA WANAWAKE UNAOFANYIKA
NEW YORK MAREKANI KUANZIA TAREHE 12- 23/03/2018
Wizara
ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inataarifu umma kuwa; Tanzania sawa na Nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa inashiriki Mkutano
wa 62 wa Hali ya Maendeleo ya Wanawake unaoendelea mjini New York, Marekani kuanzia 12 - 23 Machi,
2018.
Kwa
mwaka 2018 Kaulimbiu ya Mkutano ni “Changamoto na Fursa Katika Kufikia
Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana Wanaoishi Vijijini”.
Katika
Mkutano huo wa 62 wa Hali ya Maendeleo ya Wanawake, Tanzania inawakilishwa na Maafisa
waandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamaii, Jinsia, Wazee na Watoto;
Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto– Zanzibar; Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Wajumbe wengine ni kutoka Ofisi
ya Waziri Mkuu na Wizara ya Kilimo.
Ushiriki wa Nchi ya Tanzania kwenye Mkutano
wa 62 wa Hali ya Maendeleo ya Wanawake unaondelea Nchini Marekani unatoa nafasi
kwa washiri kufanya yafuatayo:
(i)
Kutoa maoni na mapendekezo kwenye kikao
cha majadiliano ya Mawaziri wa Masuala ya Maendeleo na Haki za Wanawake kuhusu
utekelezaji wa vipaumbele vya Kaulimbiu kuanzia tarehe 12 - 13 Machi 2018.
(ii)
Kuwasilisha
Taarifa ya Nchi kuhusu juhudi za Taifa katika kutekeleza vipaumbele vya
Kaulimbiu kwenye Kikao kilichofanyika tarehe 14 Machi, 2018.
(iii)
Kuandaa vikao kazi vilivyotoa fursa kwa
washiriki kutoa maoni kuhusu agenda ya “Jitihada za Kufikia Usawa wa Kijinsia
Nchini Tanzania” kilichofanyika tarehe 14 Machi, 2108 kwa lengo la
kubadilishana uelewa kuhusu mifano bora iliyofikiwa.
(iv)
Kushiriki midaharo mbalimbali
iliyoandaliwa na nchi na taasisi nyingine kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja
na kuiga mifano bora kwa ajili ya kuleta mabadiliko Nchini Tanzania; na
(v)
Kushiriki katika majadiliano ya
utekelezaji wa masuala, maoni na mapendekezo ya uzingatiaji wa vipaumbele
katika kuendeleza hali za maendeleo ya wanawake kwenye Mkutano wa 62 wa mwka
2018.
Jitihada zilizofanyika katika
kuwezesha kufikiwa kwa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana
Nchini Tanzania
Akitoa
ufafanuzi kwa vyombo vya habari katika Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga amebainisha
kuwa hatua mbalimbali zimechukuliwa
katika kufikia usawa wa kijinsia na
uwezeshaji wa wanawake na wasichana kiuchumi wanaoishi maeneo ya vijijini. Juhudi
zilizofanyika ni kama ifuatavyo:
(i)
Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa katika
ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara na vyanzo vya nguvu za nishati miradi
ambayo itawezesha upatikanaji wa huduma bora za usafiri kwa wananchi wakiwemo
wanawake na wasichana walioko katika maeneo ya pembezoni;
(ii)
Tanzania
inatekeleza Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Miaka Mitano wa Kutokomeza Vitendo vya
Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa lengo la kupunguza madhara ya ukatili
dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.
(iii)
Tanzania imeaandaa na kuridhia sera na
sheria ambazo zinatoa nafasi zaidi kwa wanawake na wasichana wanoishi vijijini
kuweza kupata fursa ya kunufaika na huduma za kijamii, kisiasa na kiuchumi na
hivyo kuongeza haki na usawa wa kijinsia. Kwa kipindi cha mwaka 2017, Sera ya
Mikopo na Taasisi za Fedha na Sheria ya Msaada wa Kisheria zimeandaliwa na
kufanyiwa marekebisho ili kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake.
(iv)
Tanzania imechukua hatua mbalimbali za
kuwawezesha wanawake kiuchumi ikiwa ni pamoja na utoaji wa mikopo yenye riba
nafuu, utoaji wa mbinu za ujasiriamali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake,
na kuanzisha shughuli mbalimbali zinazochochea ongezeko la kipato kwa wanawake.
Hatua hizi na nyingine nyingi zimewezesha Tanzania kutajwa na ‘Taasisi ya
Kimatifa ya Uchumi’ kuwa ni kinara wa ukuaji wa uchumi jumuishi ikiongoza kati
ya Nchi zote za Afrika kwa mwaka 2018.
(v)
Utoaji wa elimu bure kuanzia Shule ya
Msingi hadi kidato cha Nne kumechangia uwiano sawa wa kijinsia katika uandikishaji
wa wavulana na wasichana wanaojiunga na za Shule za Msingi na Sekondari;
(vi)
Tanzania imarisha huduma za afya ikiwemo
uboreshaji wa afya ya mama na mtoto katika vituo vya afya pamoja na kuanzisha
maduka ya Serikali ya Dawa kwa kuongezewa bajeti kwa kiasi cha asilimia 935.
Imetolewa na:
KITENGO
CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA
YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
0 comments:
Post a Comment