Tuesday, April 24, 2018

BILIONI 256 KUTUMIKA KUJENGA KIWANDA CHA KEMIKALI MLANDIZI


 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa tano kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa Nne kulia) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson (wa tatu kulia) na baadhi ya Viongozi wakifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kemikali cha Msufini (T) Ltd,  Mlandizi mkoa wa Pwani, leo. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Wakifurahia baada ya kuweka Jiwe la Msingi
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF, Regnald Mengi, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kemikali cha Msufini (T) Ltd,  Mlandizi mkoa wa Pwani, 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akihutubia kwa niaba ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kemikali cha Msufini (T) Ltd,  Mlandizi mkoa wa Pwani
****************************************************
SERIKALI imezindua mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kemikali za kutengeneza dawa za kusafishia maji kitakachogharimu sh. Bilioni 256.
Uzinduzi huo umefanyika eneo la Mlandizi  Msufini mkoani Pwani jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kwa niaba ya Makamu wa Rais, Samiah Suluhu Hassan.
Mwijage alisema mradi huo ukikamilika utasaidia serikali kuokoa kiasi cha  fedha kilochokuwa kikitumika kununua dawa hiyo nje za nchi.
" Mradi huo ni wa tatu kwa ukubwa Afrika   na kwa sasa tunatarajia kuzindua viwanda vingine tisa vilivyo na viwango. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

 Na ili kuhakikisha adhma ya  viwanda inafanikiwa nitatoa  eneo langu kwa ajili  kujenga jumba   la utamaduni  wa viwanda, " alisema.
Mwijage aliwataka Watanzania kujenga uthubutu wa kuwekeza kwenye viwanda ili kuchochea  mageuzi ya kiuchumi.
4Mkurugenzi wa Kiwanda  hicho,  Justine  Lumbert , alimwakikishia Rais Dk.John Magufuli kuwa anacho kikosi  mahiri nchini  kwa ajili ya jenzi wa viwanda kwa mkoa wa Pwani.
Alisema mradi  huo wa dawa ni mkubwa barani Afrika  hivyo  utaisaidia nchi kutengeneza aina  ya dawa ya Chlorine itakakayotumika kusafisha maji.
" Utengenezaji wa dawa hiyo hutumia chumvi,  sasa hakuna chumvi yoyote itakayouzwa nje ya nchi hadi mahitaji ya kiwanda hicho yatakapojitosheleza kwa sababu bidhaa zitakazotengenezwa zitakuwa na soko  la asilimia 20 ndani ya nchi na 80 nje ya nchi," alisema.
Mkurugenzi huyo ujenzi wa mradi huo utagharimu kiasi cha sh.  Bilioni 256 kwa eneo la hekari nane na utakamilika  ndani ya miezi 23.
" Tunaiomba serikali kuweka sheria na kanuni stahiki zitakazosaidia kulinda bidhaa  na malighafi  ya chumvi itakayotumiwa na mradi huu," alisema.
Lumbert  alitaja faida za mradi huo, utasaidia  kuingizia taifa fedha za kigeni, kuokoa fedha za kununulia dawa nje, kuokoa gharama za  matumizi ya kusafisha maji nchini na kuongeza ajira rasmi  kwa vijana takribani 700.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack  Kamwelwe, alimuagiza  Mkurugezi wa  Mamlaka ya  Maji  Safi na Maji taka  Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi  Cyprian  Luhemeja, ndani ya siku tatu anakutana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi  Evarist Ndikilo kwa  ajili ya ujenzi wa pipa kubwa la maji eneo la Mlandizi ili kuhakikisha yanapatikana eneo hilo kwa urahisi.
" Kwa Wizara yangu itabadilisha muundo wa ununuzi kwani tutakuwa tukinunua  ununuzi wa pamoja kuanzia  Julai mwaka huu  sasa wizara yangu haitakwenda kununua sawa ya kusafisha maji nje wakati itakuwa ikipatikana  nchini," alisema.
Kamwele alizitaja aina ya upungufu uliokuwepo katika wizara yake kuwa ni utengenezaji wa  mabomba ya chuma cha pua na dawa ya kusafisha maji kwa haraka  iliyo na uwezo wa kuzamisha  vumbi na matope kwa haraka.
Naye Mhandisi  Ndikilo alisema mradi wa kiwanda hicho  ni wa tofauti Afrika Mashariki  kwa sababu  Afrika   kinapatikana   nchi ya Misri na  Nigeria.
" Wawekezaji tambueni ya kuwa mkoa wa Pwani  uko salama  kwa hiyo msipigiwe kelele na mitandao ya kijamii.
"Kiwanda hicho kinahitaji tani 2500 ya chumvi  kwa  mwezi kwa hiyo wazalishaji changamkieni fursa hiyo  kwa sababu hakuna chumvi itakayochukuluwa nje ya nchi," alisema.
 Sehemu ya wageni waalikwa
 Wasanii wa Bendi ya JKT wakitoa burudani.....
 Baadhi ya wafanyakazi wa Junaco wakisebeneka katika hafla hiyo
 Mgeni rasmi akielekea meza kuu
 Naibu Spika akielekea Meza Kuu
 Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya zoezi la uwekaji Jiwe la Msingi. Kushoto ni Naibi Spika wa Bunge la Jamhuri, Tulia Ackson. 
 Picha za kumbukumbu baadhi ya wageni waalikwa katika jiwe la msingi, Papii Kocha akisoo love na wadau
 Picha za kumbukumbu
Picha za kumbukumbu...
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu