Tuesday, April 24, 2018

WANAWAKE NI NGUZO YA MAENDELEO KATIKA KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA - DC MCHEMBE

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe akipongezwa na mchungaji Canon Chamwenye wa kanisa Anglikana Msingisi mara baada ya kumaliza kuongea na akina mama juu ya kuanzisha kiwanda ili waweze kujikwamua katika maisha yao.
Mmoja ya akinamama akitoa shukrani ya kuku kwa mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe afanikisha ushawishi wa ujenzi wa viwanda kwa kuanzia na wanawake kanisa la Anglikana Dinari ya Rubeho Gairo. Ushawishi huo ulianza mwezi wa sita mwaka 2017 ambapo Mhe. Mchembe alihudhuria mkutano wa wanawake wa kanisa hilo akiwa Mgeni Rasmi. Katika mkutano huo Mhe. Mchembe aliwashawishi akinamama hao kupitia umoja wao waanzishe kiwanda ili kiwainue kiuchumi. Aidha wapate mahali pa kuuza mbegu za alizeti ambazo kwa sasa alizeti ni kati ya mazao makuu ya biashara wilayani Gairo. Hatimaye mpango umekamilika na Mhe. Mchembe amechangia pesa za Kitanzania shilingi laki tano kuhamasisha ujenzi wa kiwanda. Jumla ya gharama ya mradi ni shilingi milioni kumi na tisa. Majengo yanaendelea kufunguliwa na mradi unategemewa kuanza mwishoni mwa mwaka 2018. Mkuu wa Wilaya aliwashukuru wana Dinari hiyo iliyojumuisha Kata ya Rubeho na Msingisi. Wanawake ni nguzo ya Maendeleo katika uchumi wa viwanda. --
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu