Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa
Jesca Msambatavangu akiwapokea makada wa Chadema jimbo la Iringa
mjini walioamua kuachana na Chadema na kujiunga na CCM
Maandamano ya boda boda na magari katika kuhitimisha mbio za Bendera ya CCM mkoa wa Iringa
Wananchi wa maeneo ya Miyomboni eneo la mashine tatu wakishuhudia msafara wa Bendera ya CCM ukipita eneo hilo
Makada wa Chadema wakisalimisha kadi zao kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Bi Jesca Msambatavangu
Umati mkubwa wa wananchi waliojipanga barabarani wakati wa msafara wa bendera ukipita
Msafara wa bendera katika manispaa ya Iringa
Wananchi wakiwa katika mkutano wa kilele cha mbio za bendera mkoa wa Iringa
Vijana walioshiriki kukimbiza bendera ya CCM mkoa wa Iringa
Kada wa Chadema katikati Violeth Mwakisyala akiwa ameungana na wana CCM kuweka alama ya dole baada ya kujivua Chadema na kujiunga CCM
|
Kada
wa CCM Bw Julio Elieza kushoto akisoma maandishi ya CHANA GWANDA NA
GAMBA NA VAA UZALENDO mara baada ya kujiunga na CCM akitokea Chadema |
kada wa Chadema Bw Mmasi akionyesha kadi yake ya Chadema kabla ya kujiunga na CCM katika kilele cha mbio za bendera
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa akimkaribisha CCM Bi Violeth baada ya kujiengua Chadema
Makada na wapiganaji wa Chadema waliojiunga na CCM
Kiapo cha utii kwa waliojiunga na CCM kutoka vyama mbali mbali
Kiongozi mkuu wa mbio za bendera
Alli Simba akijiandaa kumkabidhi bendera diwani wa kata ya
Makorongoni Bw Thadeus Tenga ili akabidhi kwa mwenyekiti wa CCM mkoa
Tenga akijiandaa kupokea bendera toka kwa Simba
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa
Jesca Msambatavangu kulia akipokea bendera toka kwa diwani wa kata ya
makorongoni na kiongozi wa mbio hizo
Na Francis Godwin BLog,Iringa
MBUNGE
wa jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amerushiwa makombora
na baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao juzi walitimkia Chama cha
Mapinduzi (CCM).
Makombora
hayo yalirushwa katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa, wakati CCM
Mkoa wa Iringa ikihitimisha mbio zake za bendera ya CCM.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu alisema lengo la mbio za bendera ya CCM ni
kuhamasisha amani na utulivu nchini.
Malengo
mengine ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho unaofanywa na
serikali, kuhamsisha vijana kujiajiri na kuwashukuru watanzania kwa
kuendelea kuinga mkono CCM.
Katibu
Uenezi na Itikadi Mkoa wa Iringa, Dk Yahaya Msigwa alisema jumla ya
wanachama 120 kutoka vyama mbalimbali vya upinzani kikiwemo Chadema
wamerejea CCM kupitia mbio hizo.
Baadhi
ya wanachama wa Chadema waliokabidhiwa kadi zao kwenye hitimisho la
mbio hizo zilizoanza miezi miwili iliyopota ni pamoja na Ibrahim Mmasi
na Vaileti Mwakisyala.
Akirusha makombora kwa Mchungaji Msigwa, Mmasi alisema ni kiongozi asiyeambilika huku akimtuhumu kwamba ni mroho wa madaraka .
Mmasi alisema wakati wa kampeni za
Uchaguzi Mkuu wa 2010, Mchungaji Msigwa aliwatuhumu baadhi ya viongozi
akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Monica Mbega (CCM) kwa
kuwa na vyeo vingi vya kisiasa hali iliyosababisha ashindwe kutekeleza
wajibu wake kwa wananchi.
“Wananchi walimsikia Mchungaji Msigwa na
kumpa ubunge, lakini baada ya kupata nafasi hiyo anazidi kujilimbikizia
vyeo hali inayofinya demokrasia ndani ya chama,” alisema.
Akivitaja baadhi ya vyeo vya mbunge huyo,
Mmasi alisema mbali ya kuwa mbunge, Mchungaji huyo ni diwani,
mwenyekiti wa chama hicho wilaya, mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na
waziri kivuli.
Alisema hali ya kisiasa ndani ya chama
hicho wilayani hapa na mkoani kwa ujumla sio nzuri kwa kuwa hakuna
demokrasia ya kukosoa na kukosolewa.
“Kuna udikteta wa mawazo, watu wakisema ukweli wanachukiwa, mambo hayako shwari hata kidogo,” alisema.
Alisema kuna viongozi ambao hawapikiki
chungu kimoja na mchungaji Msigwa, hawasalimiani, hawaaminiani kwa kile
kinachoelezwa kwamba hapendi kukosolewa.
Huku
akishangiliwa na baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo, Mmasi
alisema kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao, Chadema mjini Iringa itakuwa
imesambaratika.
“Uchaguzi
ndani ya chama hicho umekaribia, waliopo na tuliokuwepo tunajua
kinachoendela, hali sio nzuri kwasababu wanachama walio wengi wanataka
mabadiliko, hali hiyo haitawaacha salama,” alisema.
huku wanachama zaidi ya 200 wapya
wakijiunga na chama hicho huku baada ya makada wa chama cha
Demokrsani na maendeleo (CHADEMA) wakijiengua katika chama hicho na
kujiunga na CCM.
Makada hao wa Chadema wameeleza
kufurahishwa na utendaji kazi wa serikali ya CCM na kuchukizwa kile
walichodai ni ubabaishaji wa Chadema katika ngani ya jimbo , mkoa na
Taifa kwa madai kuwa vitendo vya kifisadi ndani ya Chadema ni moja
ya sababu ya wao kujiengua.
Makada hao wakitumia muda mwingi
kushambulia mbunge wa jimbo la Iringa mjini na diwani wa Mvinjeni
na viongozi wa Chadema taifa walisema kuwa wamechoshwa na porojo
za viongozi hao.
Pia vijana hao walisema kuwa
wamekuwa wakipokea vitisho mbali mbali kutoka kwa viongozi na makada
wa Chadema pale wanapotaka kuhamia CCM
Msambatgavangu alisema kuwa CCM mkoa wa
Iringa haitawavumilia viongozi wa serikali ambao watashindwa
kutekeleza majukumu yao .
Huku ikiwatoa hofu vijana waliopo
upinzani ambao wanataka kurudi CCM kuwa wana uhuru wa kwenda chama
chochote cha siasa.
Kwa
kupitia mbio hizo za bendera Msambatavangu alisema jumla ya wanachama
wapya 4,000 wamepatikana katika wilaya zote za mkoa wa Iringa, na
wanachama zaidi ya 1,000 wamejiunga na jumuiya mbalimbali za CCM
On Wednesday, November 27, 2013 12:32 AM, Bashir Nkoromo <nkoromo@gmail.com> wrote:
CAPTIONS
1.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake (katikati) wakiwa
wamezungukwa na umati wa wananchi, Kinana alipokuwa akizindua Shina la
Wakereketwa Wajasirimali wa Kikundi cha Amani na Maendeleo cha waendesha
bodaboda, Katika Kata ya Kiwira, Rungwe mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.
2.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi nyumba ya
mwalimu katika shule ya sekondari Kaya ya Ikuti, wilayani Rungwe mkoani
Mbeya, Nov 27, 2013.
3.
Wananchi katika Kata ya Ikuti, wilayani Rungwe wakimshangilia Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Hayupo Pichani) huku wengine wakiwa juu
ya miti ili kumuona kiongozi huyo wa CCM, katika mkutano wa hadhara,
uliofanyika Nov 27, 2013, katika kata hiyo.
4. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia wananchi wa Kata ya Masoko, Rungwe, mkoani Mbeya, Nov 27, 2013.
5.
Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye akifurahia jambo na
Mbunge wa Rungwe Magharibi,Prof. David Mwakyusa, wakati wa mkutano
uliofanyika katika jimbo hilo, Kata ya Masoko, wilayani Rungwe mkoani
Mbeya, Nov 27, 2013.
5b.Katibu
wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye akimkumbatia kwa furaha Mbunge
wa Rungwe Magharibi, Prof. David Mwakyusa, wakati wa mkutano uliofanyika
katika jimbo hilo, Kata ya Masoko, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Nov
27, 2013
6.
Wananchi waliokuwa wakifanya biashara katika soko la Kata ya Ikuti,
katika kijiji cha Butonga, wilayani, Rungwe, wakiwa wameacha biashara
zao na kuzuia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana ili
kumweleza kero zao, alipokuwa akipita eneo hilo, akiwa katika ziara ya
kukagua utelezaji ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujaliana
nao njia bora ya kuzitatua, Nov 27, 2013.
7.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
akipewa zawadi na Jane James, Mke wa Mjumbe wa Shina namba 2, Butonga,
Kata ya Ikuti, Rungwe, James Mbasi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana, alipotembelea nyumbani kwa mjumbe huyo, Nov 27, 2013.
8.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpongeza kijana Asimwise
mwantebele baada ya kijana huyo kutangaza kuhamia CCM akitokea Chadema,
wakati Katibu Mkuu huyo alipokuwa akizindua shina la wakereketwa wa CCM
la Kiwira, wilayani Rungwe, Nov 27, 2013.
9.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimhoji jukwaani, Mkuu wa
wilaya ya Rungwe, Crispian Meela (kushoto) ni kwa kiwango gani
amesimamia utekelezaji wa ilani ya CCM, wilayani kwake, wakati wa
mkutano wa hadhara kata ya Ikuti, wilayani humo, mkoani Mbeya, Nov 27,
2013.
10.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na inamama wauza
ndizi wa Iponjola, wilayani Rungwe mkoaoni Mbeya, Nov 27, 2013.