CHRISTOPHER LISSA mwandishi wa sani akionyesha nyumba al;imokuwa amepanga kungolewa magati na mwenye nyumba amabye ni diwani wake
TAAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CHRISTOPHER LISSA
Dar es Salaam.
Jan, 22, 2015
0654 586788
YAH: KUVUNJIWA NYUMBA KWA GHAFLA NA MH. DIWANI WA KATA
YA MIANZINI MBAGALA
Mimi mtajwa
hapo juu ni mwandishi wa habari ninayefanya kazi katika gazeti la Sani kwa miaka minne sasa nikiwa
kama Mwandishi wa habari Mwandamizi na mpiga picha.
Ninayo masikitiko makubwa kufuatia kitendo cha Mkurugenzi
na mmiliki wa Gazeti la Sani ambaye pia ni . Diwani wa kata ya Mianzini, Mbagala Temeke kuchukua
hatua za kuivunja nyumba niliyokuwa naishi kwa ghafla huku familia yangu ikiwa
ndani hivyo kuniacha bila mahali pa
kuishi na kuruhusu mali zangu kuibiwa vikiwemo vitendea kazi.
Tukio hili alifanya
Januari 19 majira ya saa 9 alasili ambapo bila kuwa na kibali chochote, wala idhini ya Serikali ya
Mtaa, mjumbe au usimamizi wa Polisi na
pasipo kunipa Notice Mheshimiwa huyo alivamia
nyumba hiyo na kuivunja huku familia yangu ikiwa ndani.
Nyumba hiyo ipo eneo la Kokoto, mbele kidogo ya
Mbagara Rangi Tatu karibu na Shule ya St. Marys .Alinikabidhi kwa hiyari nikiwa
kama mshiriki wa kazi zake ili niweze
kuishi pamoja na familia yangu.
Kutoka tarehe niliyotaja hapo juu mpaka sasa mimi na familia yangu ya watu watano tumekuwa tukiishi nje hivyo kujikuta tukiishi kwa taabu sana .
Uamuzi wa kuivunja nyumba hiyo ulitokana na mgogoro wa
kikazi akinituhumu kwamba nimeacha kazi kwake kimyakimya jambo ambalo si kweli kwani hadi kufikia Januari 20 ,January 2015 bado nilitambulika
na bodi ya Uhariri kama Mwandishi wa
habari Mwandamizi.
Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu,
unyanyasaji pamoja na matumizi mabaya ya madaraka ambavyo amekuwa akitumia Mh. Diwani Mbwana.
Pia ni ukatili mkubwa dhidi ya wafanyakazi pamoja na
kielelezo cha jinsi waandishi wa habari hapa nchini tusivyo thaminiwa.
Ninaiomba Serikali ,na wadau kunisaidia katika kipindi
hiki kigumu kwani hivi sasa hali ni mbaya hasa upande wa
familia yangu kwani nina watoto wadogo wakiwemo wa miaka 10,5 na 2 ambao kwa takriban siku tatu sasa naishi nao nje. nikiendelea kufuatilia
taratibu za haki kuchukua mkondo wake.
Aidha tunaishi kwa hofu kutokana na Diwani huyo kunipa
tishio la mdomo kwamba ataniua tu. Mh. Diwani alitamka hayo tukiwa katika kikao
cha usuluhishi katika ofisi za Serikali ya Mtaa Kimbangulile tar 17 jan 2015
ambapo na mimi niliripoti siku hiyo hiyo katika kituo cha Polisi
Kizuiani, Temeke, na kweli alifika tar 18,jan 2015 na kujaribu kufanikisha
jaribio la kuua kwa kuvunja nyumba wakati mimi na familia tukiwa ndani .
Nalishukuru Jeshi la Polisi Temeke ambalo lilisimama
imara kuinusuru familia yangu ambayo ilikuwa ndani wakati paa la nyumba hiyo
likivunjwa huku vijana walioamrishwa na diwani huyo wakiwemo watoto wake
wakipora mali zangu na kutoweka, vikiwemo vitendea kazi vyangu vya uandishi wa habari.
(Jinsi ya kufika eneo la tukio ni
Barabara ya Kilwa kituo Mbagala
Kokoto katika kituo cha Mafuta cha
Camell. )
TAARIFA HII PAMOJA NA PICHA AMETUMA MWENYE WE Kwa maelezo zaidi
0654 58 67 88
CHRISTOPHER LISSA
|
Dah huruma sana
ReplyDelete