Thursday, January 22, 2015

MWANDISHI WA HABARI ALALA NJE NA FAMILIA BNAADA YA NYUMBA KUNGOLEWA MABATKI






CHRISTOPHER LISSA mwandishi wa sani akionyesha nyumba al;imokuwa amepanga kungolewa magati na mwenye nyumba amabye ni diwani wake
TAAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CHRISTOPHER LISSA
Dar es Salaam.
Jan, 22, 2015
0654 586788
YAH: KUVUNJIWA NYUMBA KWA GHAFLA NA MH. DIWANI WA KATA YA MIANZINI MBAGALA
Mimi  mtajwa hapo juu  ni mwandishi wa habari  ninayefanya kazi katika  gazeti la Sani kwa miaka minne sasa nikiwa kama Mwandishi wa habari Mwandamizi na mpiga picha.
Ninayo masikitiko makubwa kufuatia kitendo cha Mkurugenzi na mmiliki  wa Gazeti  la Sani ambaye pia ni  . Diwani  wa  kata ya Mianzini, Mbagala Temeke kuchukua hatua za kuivunja nyumba niliyokuwa naishi kwa ghafla huku familia yangu ikiwa ndani hivyo kuniacha bila mahali   pa kuishi na kuruhusu mali zangu kuibiwa vikiwemo vitendea kazi.
Tukio hili alifanya  Januari 19 majira ya saa 9 alasili ambapo bila kuwa na  kibali chochote, wala idhini ya Serikali ya Mtaa, mjumbe au usimamizi wa Polisi  na pasipo kunipa Notice Mheshimiwa huyo alivamia  nyumba hiyo na kuivunja huku familia yangu ikiwa ndani.
Nyumba hiyo ipo eneo la Kokoto, mbele kidogo ya Mbagara Rangi Tatu karibu na Shule ya St. Marys .Alinikabidhi kwa hiyari nikiwa kama mshiriki wa kazi zake  ili niweze kuishi pamoja na familia yangu.
Kutoka tarehe niliyotaja hapo juu  mpaka sasa mimi na familia yangu ya watu  watano tumekuwa tukiishi nje  hivyo kujikuta tukiishi kwa taabu sana  .
Uamuzi wa kuivunja nyumba hiyo ulitokana na mgogoro wa kikazi  akinituhumu kwamba  nimeacha kazi kwake kimyakimya  jambo ambalo si kweli kwani hadi kufikia  Januari 20 ,January 2015 bado nilitambulika na bodi ya Uhariri  kama Mwandishi wa habari  Mwandamizi.
Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, unyanyasaji pamoja na matumizi mabaya ya madaraka ambavyo  amekuwa akitumia Mh. Diwani  Mbwana.
Pia ni ukatili mkubwa dhidi ya wafanyakazi pamoja na kielelezo cha jinsi waandishi wa habari hapa nchini tusivyo thaminiwa. 
Ninaiomba Serikali ,na wadau kunisaidia katika kipindi  hiki kigumu  kwani hivi sasa hali ni mbaya hasa upande wa familia yangu kwani nina watoto wadogo wakiwemo wa miaka 10,5 na 2  ambao kwa takriban siku tatu sasa  naishi nao nje. nikiendelea kufuatilia taratibu za haki kuchukua mkondo wake.
Aidha tunaishi kwa hofu kutokana na Diwani huyo kunipa tishio la mdomo kwamba ataniua tu. Mh. Diwani alitamka hayo tukiwa katika kikao cha usuluhishi katika ofisi za Serikali ya Mtaa Kimbangulile tar 17 jan 2015 ambapo na mimi niliripoti    siku hiyo hiyo katika kituo cha Polisi Kizuiani, Temeke, na kweli alifika tar 18,jan 2015 na kujaribu kufanikisha jaribio la kuua kwa kuvunja nyumba wakati mimi na familia tukiwa ndani .
Nalishukuru Jeshi la Polisi Temeke ambalo lilisimama imara kuinusuru familia yangu ambayo ilikuwa ndani wakati paa la nyumba hiyo likivunjwa huku vijana walioamrishwa na diwani huyo wakiwemo watoto wake wakipora mali zangu na kutoweka, vikiwemo vitendea kazi vyangu  vya uandishi wa habari.
(Jinsi ya kufika eneo la tukio  ni  Barabara ya Kilwa  kituo Mbagala Kokoto  katika kituo cha Mafuta cha Camell. )
TAARIFA HII PAMOJA NA PICHA AMETUMA MWENYE WE Kwa maelezo zaidi
0654 58 67 88
CHRISTOPHER LISSA

na

Share this article :

1 comments:

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu