|
Karama Nyilawila
|
BONDIAw a ngumi za kulipwa nchini, Karama Nyilawila aliyewahi kuwa bingwa wa dunia wa WBF uzito wa middle anatarajiwa kupanda ulingoni mwezi ujao kuzipiga na Sado Philemon.
Nyilawila
aliyempiga Kreshnik Qato wa Czech wakati akitwaa taji lake la WBF
ambalo alilitema baada ya kushindwa kwenda kulitetea ili apate nafasi ya
kuzipiga kirafiki na Francis Cheka mjini Morogoro na kudundwa,
atazipiga na Philemon kwenye ukumbi wa CCM Mwinjuma siku ya Oktoba 20,
pambano lililoandaliwa na kampuni ya Bigright
Promotion.
Mratibu wa pambano hilo, Ibrahim kamwe alisema kuwa
maandalizi mpaka sasa yanaenda vizuri.
Hata
hivyo Kamwe alisema mabondia wanaendelea kujifua kimkandamkanda
kutokana na kukosekana kwa wadhamini na hasa mabondia watakaosindikiza
pambano hilo.
Kamwe
alisema Nyilawila na mwenzake wameshasaini makubaliano ya kupanda
ulingoni siku hiyo ambapo watasindikizwa na michezo kadhaa
itakayohusisha mabondia chipukizi.