Home » Archives for July 2014
Thursday, July 31, 2014
Wednesday, July 30, 2014
BREKING NEWZZZZZZ WATU 17 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI
BREKING NEWZZZZ WATU 17 WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE WAMEJERUHIWA
Abiaria wapatao 17 wamefariki dunia papohapo wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya basi la Moro Best lililokuwa likitokea mpwapwa kuelekea Dar essalaam kugongana uso kwa uso na Lori la Mizigo katika eneo la Panda Mbili Dodoma ajali hiyo mbaya ilitokea leo habari zinasema ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa lori kutaka kulipita lori jingine kutokana mwendo kasi ndipo ilipogongana usoso na maderevawsoto wa wili wamefariki papo hapo
Tuesday, July 29, 2014
SALA YA IDD FITRI IMEADHIMISHWA LEO
baadhi ya mabalozi wakiwa katika sala ya idd |
waumini wakiwa katika ibada ya sala ya idd |
baadhi ya waumini wa kiioslama wakisalimia Rais wa zanzibar Dr Ali Mohamed Shen |
waumini wa kiislama wakiwa kwenye sala ya Iddi mjini dodoma leo |
rais jakaya kikwete akisalimiana na waumini wa dini ya kiislama mara baada ya sala ya Idd iliyoadhimishwa leo |
Rais jakaya kikwete akisalimiana nawatoto pamoja na waumini wa kiislama mara baada sala ya Idd leo |
Rais jakaya kikwete akisalimiana na waumini wa kiislama mara baada sala ya Idd leo |
Monday, July 28, 2014
WATUHUMIWA WA KESI YA HOSPITALI YA IMTU YA KUTUPA MIILI YA BINADAMU KATIKA MACHIMBO YA KUNDUCHI WAKIWA KATIKA MAHAKAMA YA KINONDONI LEO
watuhumiwa wa IMTU wakitoka katika mahakama ya kinondoni kuelekea kupanda difenda kuelekea polisi ambao wanadaiwa kutupa viungo vya binadam na kutovifukia vilivyokutwa katika machimbo ya kunduchi |
watuhumiwa wa IMTU wakipanda gari la polisi baada ya kesi yao inayodaiwa kutupa viungo vya binadamu bila kufukia katika machimbo ya kunduchikesi |
watuhumiwa wakisindikizwa na poli katika mahakama ya kinondoni kesi ya inayowakabili ya kutofukia miili ya binadamu iliyotupwa katika machimbo ya kunduchihivi karibuni |
Saturday, July 26, 2014
*KATIBU WA BUNGE MAALUM AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Katibu wa Bunge Maalum la Katiba, Yahaya Khamis akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani ) kuhusu kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ndogo za Bunge jijini Dares Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu wa Bunge Maalum la Katiba, Yahaya Khamis akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani ) kuhusu kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ndogo za Bunge jijini Dares Salaam. Picha na Magreth Kinabo - MAELEZO
****************************************
****************************************
*SITTA - BUNGE MAALUM LA KATIBA KUENDELEA
Na Winner Abraham na Rose Masaka-MAELEZO-Dar es salaam
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta, amesema kuwa Mkutano wa Bunge hilo, utaendelea kama ulivyopangwa Agosti 5, mwaka huu mjini Dodoma.
Amesema kuwa licha ya baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo, kuendelea na msimamo wao wa kutaka kususia vikao vitakavyoanza mapema mwezi ujao, lakini bado kuna mambo muhimu ya kujadiliwa.
Mwenyekiti
huyo ametoa kauli hiyo leo mjini Dar es salaam, katika taarifa yake
iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba, Yahaya
Khamis wakati wa mkutano wa waandishi wa habari.
“Kamati hiyo, imeamua kupendekeza kwa Kamati ya Uongozi kwamba Bunge Maalum la Katiba liendelee kwa sababu yapo
masuala mengi muhimu ya kikatiba ambayo yanatuunganisha kama vile usawa
wa kijinsia katika nafasi za uongozi na kuikarabati Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).
“Mambo
mengine ni kurekebisha kikatiba masuala ya Muungano,haki za
wakulima,wafugaji,wasanii na makundi mengineyo na ukomo wa vipindi vya
uongozi,”alisema Sitta katika taarifa hiyo.
Aidha aliongeza kwamba uamuazi huo, umefikiwa baada ya wajumbe wa Kamati hiyo waliohuduria ambao walikuwa zaidi ya theluthi mbili ya wajumbe wote, ambapo waliendelea na kikao.
Alisema hatua
ya baadhi ya wajumbe kwenda kwa wananchi na maoni yao imekuwa siyo
muafaka na si wakati wake, hivyo Bunge hilo liwajibike katika siku za
usoni kujibu upotoshwaji wowote kuhusu mchakato wa katiba kadri
unavyojitokeza.
Aliongeza kwamba Kamati hiyo, inaona kwamba
kwa kuendelea kulisusia Bunge hilo, na kupuuza wito wa jamii kupitia
makundi mbalimbali pamoja na madhehebu ya dini inatilia shaka dhamira
halisi ya viongozi wa kundi hili la wasusiaji kupuuzia juhudi zote za usuluhishi, kunazua mashaka kuhusu lengo la ususiaji kwamba pengine agenda ya viongozi hawa ni nyingine na siyo upatikanaji wa Katiba.
Alisema Kamati hiyo inarejea kwamba wajumbe hao 629
wamekabidhiwa jukumu adhimu na la kihistoria kwa niaba ya Watanzania
jukumu ambalo hutokea baada ya miongo kadhaa ya uhai wa Taifa lolote.
“ Tutakuwa hatuwatendei haki Watanzania ikiwa hatutafikia maridhiano yanayotuwezesha kukamilisha kazi tuliyopewa,” alisisitiza.
Mwenyekiti huyo alisema katika ngwe ya pili inayoanza mapema mwezi ujao mkutano wa Bunge hilo, uzingatie upya baadhi ya Kanuni za Bunge hilo, ambazo ni kikwazo katika kuhakikisha kwamba kazi ya kujadili na hatimaye inayopendekezwa inakamilika ndani ya siku 63 zilizosalia kisheria, kati ya hizo siku 60 ni za nyongeza na tatu zilizokuwa pungufu za siku 70 za awali.
Alisema
Kamati hiyo, inaendelea kutoa wito wa wajumbe waliosusia mikutano ya
Bunge hilo, kurejea katika Bunge hilo, ambalo pekee ndiyo lina uwezo wa
kisheria wa kutatua matatizo yaliyopo.
Amesema
kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 54 kifungu cha nne na tano ya Kanuni za
Bunge Maalum la Katiba, aliteua Kamati ya Mashauriano ya wajumbe
thelathini (30) kujadili matatizo yaliyojitokeza Dodoma katika mkutano
ulipita lakini wajumbe kutoka Chama cha CUF, CHADEMA na NCCR
Mageuzi,walikisusa kikao cha jana Julai 24 mwaka huu.
“Jitihada mbalimbali zilizofanywa na sekretarieti pamoja na mwenyekiti hadi asubuhi ya siku ya mkutano hazikuweza kuwashawishi wajumbe hao wasusiaji kuhudhuria kikao, alisema Sitta katika taarifa yake.
Aliitaja athari za kutoendelea na mchakato uliopangwa wa kuandaa na hatimaye kuipigia kura Katiba mpya ni pamoja na kupoteza mabilioni ya fedha za wananchi zilizokwisha tumika katika kazi, baya zaidi ni kuiweka rehani amani ya nchi yetu kwa kuukuza mno mgogoro wa katiba na kuwagawa wananchi kwa propaganda hadi uchaguzi mkuu 2015.
RAIS JAKAYA KIKWETE AHUDHURIA MAHAFALI YA KOZI YA PILI YA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI TAASISI MALUUM UTOAJI MAFUNZO YA USALAMA WA KITAIFA NA KIMATAIFA
Profesa ibrahim lipumba akisalimiana na mkuu wa majeshi ya ulinzi David Mwamunyange wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha jeshi NDC |
MKUU WA JESHI LA POLISI MANGU AKIWA NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MECK SADIK |
RAIS JAKAYA KIKWETE AKIONGEA NA WAKUU WA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA |
RAIS JAKAYA KIKWETE AKISALIMIANA NA ERNEST WAMBA DIA WAMBA |
RAIS JAKAYA KIKWETE AKIFURAHIA JAMBO PAMOJA NA DR BANA NA PROFESA IBRAHIM LIPUMBA |
WAHITIMUWA JESHI |
RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWA NA WAHITIMU WA MAHAFALI |
RAIS AKIWA NA WATU MBALIMBALI |
WAHITIMU WA CHUO CHA JESHI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA |
RAIS JAKAY KIKWETE AKIELEKEA KATIKA JUKWAA |
RAIS AKIONGEA NA BAADHI YA MABALOZI |
RAIS JAKAYA KIKWETE AKIAGANA WAKUU WA JESHI LA ULINZI |
RAIS JAKAY KIKWETE AKIELEKEA KATIKA JUKWAA |
BAADHI YA WANAJESHI WAHITIMU KATIKA CHUO CHA JESHI WAKATI WA MAHAFALI YA PILI YA CHUO HICHO |
BAADHI YA WANAJESHI WAHITIMU KATIKA CHUO CHA JESHI WAKATI WA MAHAFALI YA PILI YA CHUO HICHO |
RAIS JAKAYA KIKWETE AKIWAAGA WAHITIMU WANAJESHI WA CHUO CHA JESHI LEO |
RAIS JAKAYA KIKWETE AKIFURAHI KITUPAMOJA NA WAGENI MBALIMBALI |
SHIWATA yaipongeza Serikali kutambua kijiji chao Mkuranga
SERIKALI imepongezwa kwa kutambua juhudi zinazofanywa na wasanii, wanamichezo na waandishi wa habari za kujenga nyumba za makazi katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga ambapo Mwenge wa Uhuru ulifika na kuweka jiwe la msingi Julai 22 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib katika risala aliyosoma mbele ya Kiongozi wa Mwenge kitaifa, Rachael Kassanda alisema Serikali kukitambua kijiji hicho kumeongeza ari ya wasanii kujenga nyumba za kisasa na kuongeza kasi ya maendeleo.
Alisema kijiji cha wasanii kimeanzishwa mahususi kwa ajili ya kuwakomboa na kuwapatia makazi ya kudumu wakisha staafu au kupotea kwa umaarufu wao katika fani zao.
Katika sherehe hizo ambazo wasanii zaidi ya 1,500 waliofurika kupokea mwenge wa uhuru kiongozi wa mbio za Mwenge, Rachael Kassanda aliwatoa wito kwa wasanii kuwa kioo halisi cha jamii kwa kuiga mema na kupiga vita mabaya katika jamii zinazowazunguka.
Awali Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila aliwaasa wasanii kutumia vipaji vyao kuwaelimisha jamii kuhusu maadili mema na kuiga yanayostahili kwa mila na desturi za Mtanzania.
Katika sherehe za kuweka jiwe la msingi zilizofanywa na kiongozi wa mbio za Mwenge,SHIWATA ilimsimika balozi wa kijiji hicho kuwa ni msanii maarufu na mtangazaji wa kituo cha Redio Times FM, Suzan Natasha ambaye aliahidi kukitangaza kijiji hicho katika mipaka ya ndani na nje ya Tanzania.
Sherehe hizo zilizoambatana na burudani mbalimbali zilizongozwa na Bendi ya Polisi, wanamuziki maarufu Kikumbi Mwanzo "King Kikii", Siza Mazongera "Wana Segere" na wasanii mbalimbali walitumbuiza.
Wengine walioshudia kuwekwa jiwe la msingi katika kijiji hicho baadhi yao ni wachezaji wa zamani wa Simba, Moses Mkandawile, George Lucas,Thom Kipese na kwa upande wa Yanga ni Abeid Mziba, Ramadhani Kampira, Bakari Malima, Omari Husein na wengineo.
Pia katika kusherekea mwenge wa uhuru SHIWATA ilitoa ofa bure kwa wanachama wapya kupimiwa viwanja vya kujenga nyumba bure katika kijiji hicho ambapo wanamichezo, wasanii na waandishi wa habari walipata fursa ya kuoneshwa viwanja watakavyotakiwa kujenga.
mwisho
BREAKING NEWS : BASI LA HOOD LAPATA AJALI MBAYA ASUBUHI HII LIKITOKEA MBEYA
Muda mchache baada ajali kutokea
Askari wa usalama wa barabarani wakiwa wamefika eneo la tukio na baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo
Basi
la Hood limepata ajali asubuhi hii likitoka Mbeya haijafahamika mara
moja lilikuwa linaelekea wapi na haijafahamika kama kuna watu
waliojeruhiwa, endelea kufutilia hapa kupata taarifa kamili hii ni
taarifa ya awali.
Picha na Mbeya yetu Blog
Friday, July 25, 2014
MKUTANO KATI YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM NA WANAMTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA NA TAMWA LEO
Usu Millya Mwanamtandao wa Ulingo wa Katiba na wanawake ambaye alikuwa ndiye mwezeshaji wa Mkutano huo ambao ulikuwa ni wa siku mbili akiendelea kutoa mwongozo wa mkutano huo.
Doreen E. Maro kutoka TAMPRODA ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba akiwakilisha Wafugaji Akileta Mrejesho wa walichokuwa wakikijadili katika Kundi lao juu ya mapendekezo ya kuimarisha Masuala muhimu ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya
Dkt. Macca A. Mbalwa Mkurugenzi wa Giyedo Tanzania akiwa anatoa Mrejesho wa kile ambacho walikuwa wamekijadili na kutoa mapendekezo yao ya Kuboresha masuala muhimu katika Rasimu ya pili ya Katiba Mpya.
Salama Aboud Talib Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Naibu Katibu Mkuu wa UWT akizungumzia makosa mbalimbali ambayo yapo katika Rasimu ya Pili ya Katiba mpya na kutoa mapendekezo kuwa Iboreshwe ili kuweka usawa.
Executive Director wa Women Fund Tanzania Mary Rusimbi akizungumza juu ya Majumuisho ya pomoja na Kupanga mikakati ambayo yatasaidia Kuimarisha Masuala Muhimu ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya
Mgeni Hassan Juma Mwenyekiti wa Wawakilishi Wanawake Zanzibar akitoa neno la Shukurani kwa wote waliohudhuria kwa muda wa siku mbili katika mkutano wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mtandao wa wanawake na TAMWA
Profesa Ruth Meena Akitoa Majumuisho pia kutoa Shukurani kwa wale wote waliohudhuria katika Mkutano huo uliochukua siku mbili.
Valerie Msoka akifunga Rasmi Mkutano huo.
Fredrick Msigala Mjumbe Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mlemavu wa Miguu akielezea masikitiko yake ya Jinsi watu wenye ulemavu wakiwemo wanawake na wanaume ambavyo wametengwa na kukosa haki zao, amesisitiza Serikali katika Rasimu Mpya ya Pili ya Katiba wawaangalie walemavu kwa umakini na ukaribu maana wanahaki sawa na watu wengine. Pia amesisitiza walemavu wajaliwe katika huduma za Afya mana ni Muhimu kwao. Mwisho amesisitiza kuwa wanawake wenye ulemavu wanahaki ya Kuolewa na kuto nyanyaswa pindi wanapokuwa katika ndoa zao.
Modesta Mpereme ambaye ni Kiziwi hasikii lakini anaongea vizuri pia ni Mwenyekiti kutoka Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania, Ameiomba serikali iwe na vitendea kazi vya kutosha ambavyo vitawasaidia walemavu katika secta mbalimbali Mfano katika Mabenki kuwe na vifaa maalum vya kuwasaidia walemavu, Katika Upande wa Afya amesisitiza kuwe na hata watu wanaoweza kutoa msaada wa kutafsiri mambo mbalimbali mfano kwa Viziwi, wasio ona na ambao Hawawezi kuongea.
Siti Ally Mwanasheria na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar akisisitiza umuhimu wa usawa kati ya haki za wanawake na wanaume katika jamii , Pia alisisitiza juu ya mabinti wanaopata Mimba za utotoni wakiwa mashuleni na kusisitiza kuwa wanaruhusiwa kusimama masomo mpaka kipindi mtoto atakapokuwa mkubwa anaruhusiwa kuendelea na masomo, Mwanaume aliyesababisha Mimba anaweza akashtakiwa .
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba pamoja na Wadau mbalimbali waliofika katika Mkutano huo.
Subscribe to:
Posts (Atom)