Thursday, January 31, 2013

0 comments

BREAKING NEWS: DIZUMBA WA MAJIMAJI AFARIKI

HABARI zilizotufikia muda huu zinasema kuwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Majimaji Songea inayojiandaa na duru la pili la Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, Ahmed Dizumba amefariki dunia.
Taarifa zilizopatikana  leo asubuhi  ambazo  inaendelea kuzifuatilia kwa ukaribu zinasema Dizumba amefariki usiku wa kuamkia leo na anatarajiwa kuzikwa leo mjini Songea.
Kwa yeyote mwenye taarifa zaidi anaweza kutupenyezea, juu ya msiba huu ulioikumba Majimaji ikiwa katika harakati za kuanza duru la pili la ligi daraja la kwanza kuwania kurejea ligi kuu.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TFF, Majimaji imepangwa kuanza utepe wa duru hilo kwenye uwanja wake wa Majimaji Songea kuvaana na Kurugenzi mechi ya kundikwa niaba ya blog ya micharazo
Endelea Kusoma >>

KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

0 comments
Mbunge wa kuteuliwa, Jamsi Mbatia, akitumia moja ya vitabu kadhaa vya ziada na kiada, bungeni mjini Dodoma, alivyoleta kama kielelezo cha hoja yake binafsi ya udhaifu ulioko kwenye sekta ya elimu nchini. Kushoto ni mbunge wa Mhambwe, Felix Mkosamali.
Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Kulia) na mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu, wote kutoka CHADEMA, wakimlalamikia spika wa bunge Anne Makinda, wakati akiongoza kikao cha bunge jana mjini Dodoma ambapo mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia, alitoa hoja binafsi kuhusu udhaifun ulioko katika sekta ya elimu nchini
Endelea Kusoma >>
0 comments



MAAMUZI KUHUSU PINGAMIZI DHIDI YA WAOMBAJI UONGOZI

WA TFF NA TPL BOARD



31 JANUARI 2013



Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(4) katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Januari 2013, ilijadili pingamizi zilizowekwa dhidi waombaji uongozi wa TFF na TPL Board na kutoa maamuzi kama ifuatavyo:



1.                   Waombaji uongozi wa TPL Board



(a)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Said Muhammed Abeid anayeomba kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na  Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg. Said Muhammed, aliyeoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Said Muhammed:



(i)                   Si Mwenyekiti wa Klabu ya Azam na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.

(ii)                 Si mkweli katika maelezo aliyoyatoa kwenye fomu yake ya maombi ya uongozi.



Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia maelezo ya Mweka pingamizi na ilijiridhisha kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Mchaki haikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa haikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi  hiyo.





(b)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Yusufali Manji anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa  na  Ndg. Daniel T. Kamna na  Ndg. Juma Ally Magoma walioomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF  kumwondoa mwombaji uongozi kugombea nafasi aliyoomba, kwamba Ndg. Yusufali Manji :



(i)                   Hana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) wa uendeshaji wa mpira wa miguu.

(ii)                 Hana sifa ya kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja la kwanza.

(iii)                Hana elimu ya kidato cha nne

(iv)               Ameshindwa kusimamia katiba ya Young Africans Sports Club Ibara ya 10(6), 18(1)b, 27 (2) na (5).



Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele yake na Ndg. Daniel T. Kamna na Ndg. Juma Ally Magoma hazikukidhi matakwa Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kuwa hazikuambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa pingamizi hizo. 



(c)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Hamad Yahya Juma anayeomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPL Board): Kamati ilijadili pingamizi iliyowasilishwa na Ndg. Frank M. Mchaki dhidi ya Ndg.  Hamad Yahya Juma, kwamba Ndg. Hamad Yahya Juma:



(i)                   Si Mwenyekiti wa Klabu ya Mtibwa na hivyo hana sifa za kugombea uongozi wa TPL Board.

(ii)                 Si mkweli na mwadilifu na amekuwa akijipachika cheo cha mwenyekiti wa klabu.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitupa pingamizi ya Ndg. Frank M. Mchaki kwa kuwa pingamizi iliyowasilishwa mbele yake haikukidhi matakwa  ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.



2.                   Waombaji uongozi wa TFF



(a)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani K. Kambi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 9 (Mtwara na Lindi): Ndg. Kambi aliwekewa pingamizi kwamba amefanya Kampeni kabla ya muda uliopangwa.



Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg. Jeremiah John Wambura kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi.





(b)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Eliud P. Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 7 (Iringa na Mbeya): Ndg. Mvella aliwekewa pingamizi na Ndg. Said Kiponza, Ndg. Abu Changawa na Ndg. Peter Naminga, kwamba Ndg. Mvella:


(i)                   Akiwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda hiyo ameshindwa kuleta maendeleo ya soka katika ukanda huo.

(j)                   Ana kesi ya rushwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa



Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) kwa kutoambatanishwa na vielelezo vyovyote kuthibitisha maelezo ya pingamizi.



(c)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Epaphra Swai anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 3 (Shinyanga na Simiyu): Kamati ilijadili pingamizi zilizowasilishwa na Ndg. Ramadhani Sesso na Ndg. Tsotsie Chalamila, kwamba Ndg. Epaphra Swai:



(i)                   Alifanya ubadhilifu wa fedha alipokuwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA).

(ii)                 Alitumia madaraka yake vibaya alipokuwa MZFA kujinufaisha kwa kutumia MZFA.

(iii)                Alivunja Katiba ya MZFA na FIFA

(iv)               Anavuruga shughuli za uendeshaji mpira wa miguu mkoani Simiyu.



Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia pingamizi hizo na ilijiridhisha kuwa wawekaji pingamizi hawakuwa na sababu za msingi zilizoambatana na vielelezo vinavyothibitisha maelezo ya pingamizi na kuwa pingamizi zilizowasilishwa mbele yake zina chembechembe za wazi za mapatano ya hila na udanganyifu (collusion) dhidi ya Ndg. Epaphra Swai. Kwa kutokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2) na hila/udanganyifu kwa Kamati, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imezitupa pingamizi hizo.



(d)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Vedastus F.K Lufano na Ndg. Mugisha Galibona wanaoomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 2 (Mwanza na Mara): Ndg. Lufano na Ndg. Galibona waliwekewa pingamizi  na Ndg. Paul Mhangwa kwamba  hawana uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu wa miaka mitano (5).



Kamati imeitupa pingamizi hiyo kwa kuwa haikuzingatia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).





(e)                 Pingamizi dhidi ya Ndg. Michael R. Wambura anayeomba kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF: Pingamizi ziliwasilishwa na Ndg. Said Rubea Tamim na Ndg. Josea Samuel Msengi kwamba Ndg. Wambura:



(i)                   Alikiuka Katiba ya TFF kwa kuishitaki Klabu yake ya Simba mahakamani kuhusu masuala ya uchaguzi.

(ii)                 Alikosa uadilifu kwa kutumia kampuni yake binafsi kufanya biashara na Taasisi aliyokuwa aniongoza akiwa Katibu Mkuu wa FAT.

(iii)                Amekuwa akijaribu kupotosha umma kwamba vyombo vya TFF havifanyi kazi zake kwa kutumia haki na kuviita ‘Mahakama za Kangaroo (Kangaroo Courts).

(iv)               Mwaka 2004 alikiri kwamba alikuwa akiandikwa vizuri na vyombo vya habari kwa kuwa alikuwa akivipa pesa na kwamba vyombo vya habari vilimgeuka kwa sababu aliacha kuwapa waandishi pesa.

(v)                 Mwaka 2004 alikataa kutekeleza maagizo ya FIFA ya kutaka nafasi ya Katibu Mkuu wa FAT iwe ya kuajiliwa.

(vi)               Alikosa uwezo wa kutekeleza wajibu na malengo ya TFF.



Ndg. Josea Samuel Msengi aliondoa pingamizi lake dhidi ya Ndg. Wambura. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Said Rubea Tamim kwa kuwa halikukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 11(2).



(f)                  Pingamizi dhidi ya Ndg. Jamal E. Malinzi anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF; Aliwekewa Pingamizi na Ndg. Agape Fue kwamba:



(i)                   Alivunja Katiba ya TFF kwa kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha kuwa wanachama wa TFF kikiwemo Chama chake cha Mkoa wa Kagera haviheshimu wala kutekeleza maagizo ya TFF, CAF, CECAFA na FIFA baada ya Kamati ya Utendaji ya TFF kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba kwa njia ya Waraka, ambayo yalihusisha pia  maagizo ya FIFA na CAF

(ii)                 Hana sifa ya uzoefu wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.

(iii)                Anakosa uadilifu na haiba ya kuliwakilisha Shirikisho nje na ndani.





Kamati imeitupa pingamizi ya Ndg. Agape Fue kwa kuwa mweka pingamizi hakutokea wakati alipotakiwa kufika kwenye Kamati ya Uchaguzi kutoa utetetezi wake kuhusu pingamizi hilo.



(g)                Pingamizi dhidi ya Ndg. Athumani J. Nyamlani anayeomba kugombea nafasi ya Rais wa TFF: Ndg. Nyamlani aliwekewa pingamizi na  Ndg. Mintanga Yusuph Gacha na Ndg. Medard Justiniani kwamba:



(i)                   Ni Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Tanzania na kwa maana hiyo ni mtumishi wa umma hivyo alikosa kigezo na sifa ya kugombea nafasi ya urais wa TFF.

(ii)                 Anakatazwa na Judicial Service Act, Public Service Act 2002 na Code of Conduct for Judicial Officers of Tanzania kugombea nafasi aliyoomba ya Rais wa TFF.

(iii)                Kutakuwa na Mgoganao wa kimaslahi endapo Ndg, Nyamlani atachaguliwa kuwa Rais wa TFF.

(iv)               Amekosa umakini na uadilifu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na kusababisha Akanunti za TFF kufungiwa na TRA.



Ndg. Mintanga Yusuph Gacha hakufika kutetea Pingamizi lake ni hivyo halikujadiliwa na Kamati. Kamati imelitupa pingamizi la Ndg. Medard Justiniani kwa kuwa alishindwa kuithibitishia Kamati kuwa alikuwa na ufahamu wa kutosha wa pingamizi lake ikiwa ni pamoja na viambatanisho vyake, hali iliyotanabaisha kuwa pingamizi hilo lilikuwa na chembechembe nyingi za hila na udanganyifu.







Angetile Osiah

KATIBU

KAMATI YA UCHAGUZI
Endelea Kusoma >>
0 comments
KIM ATEUA 21 STARS WA KUIVAA CAMEROON

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).



Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.



“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.



“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.



Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.



Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).



Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).



Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Endelea Kusoma >>

Wednesday, January 30, 2013

RAIS KABILA ATUA JIJINI DAR

0 comments

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo



  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiangalia ngoma za utamaduni alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar es salaam  mchana wa leo
Endelea Kusoma >>

CAMEROON KUIVAA STARS UWANJA WA TAIFA

0 comments



TAIFA STARS KUIKABILI CAMEROON ‘FIFA DATE’

Tanzania (Taifa Stars) itacheza na Cameroon katika moja ya mechi za kirafiki za Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date zitakazofanyika duniani kote Februari 6 mwaka huu.



Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Kikosi cha Cameroon kinachoundwa na wachezaji wengi wa kulipwa wanaocheza katika nchi mbalimbali duniani kitaanza kuwasili nchini Februari 3 mwaka huu.



Nchi kadhaa ziliomba kucheza na Taifa Stars katika tarehe hiyo ya FIFA, lakini Kocha wa Stars, Kim Poulsen ameamua kucheza mechi hiyo dhidi ya Cameroon ambayo nahodha wake ni mchezaji nyota wa kimataifa, Samuel Etoo Fils.



Congo Brazzaville, Equatorial Guinea, Rwanda na Swaziland nazo zilikuwa zimeomba kucheza dhidi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager. Ukiondoa Swaziland iliyotaka mechi hiyo ichezwe Dar es Salaam, nyingine zilitaka kucheza nyumbani kwao.



Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen atakutana na Waandishi wa Habari kuzungumzia maandalizi ya mechi hiyo ikiwemo kutaja kikosi ambacho atakitumia. Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).





Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Endelea Kusoma >>

Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

0 comments



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

   

    PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.
Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania. 
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
Endelea Kusoma >>

mbunge godbles lema wakikumbatiana na Wasira bungeni leo

0 comments
 Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema (Kushoto), akikumbatiana na waziri wan chi ofisi ya rais, Steven Wasira, alipowasili jana kwen ye bunge mjini Dodoma kwa mara ya kwanza baada ya kukaa nje kufuatia ubunge wake kutenguliwa na mahakama ya mjinin Arusha, kabla ya mahakama kuu ya Tanzania kutengua uamuzi huo wa mahakama ya chini mwishoni mwa mwaka

Kiongozi wa upinzani bungeni ambaye pia ni mbunge wa Hai, mkoani Kilimanjaro, Freeman Mbowe (Kushoto), akiteta jambo na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema, bungeni mjini Dodoma jana. . Lema ameanza rasmi shughuli zake za kibunge jana, baada ya kukaa nje muda mrefu, kufuatia uamuzi wa mahakama ya mkoani Arusha kutengua ushindi wake, kabla ya mahakama kuu ya Tanzania, kutengua uamuzi wa mahakama hiyo ya chini mwishoni mwa mwaka jana, na kumrejeshea ubunge wake
Endelea Kusoma >>

Tuesday, January 29, 2013

LULU AACHIWA KWA DHAMANA, AANGUA KILIO MAHAKAMANI

0 comments


 Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akishuka kutoka katika gari lililomleta leo Mahakama Kuu wakati wa kukamilisha taratibu za kupata dhamana. (Picha na Habari Mseto Blog) 
Lulu akiingia Mahakamani huku akisindikizwa na Askari Magereza
Lulu akiingia mahakamani huku akitabasamu.
Lulu akiingia mahakamani.
Lulu akiwa amezungukwa na baadhi ya waandishi wa habari waliotala kufanya nae mahojiano mfupi baada ya kupata dhamana.
Lulu akiangua kilio baada ya kushindwa kuongea na waandishi wa habari waliokusanyika mahakamani hapo.
Lulu akitoka katika lango Kuu la Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kupata dhamana.
Lulu akilia wakati akitoka Mahakamani huku nyumba akifuatiwa na mama yake mzazi.pamoja na dr cheni
Wasanii nao wallijitokeza mahakamani hapo kumfariji Lulu, kulia ni msanii wa filamu, Muhsin Awadh 'Dk. Cheni'
Lulu akiondoka mahakama hapo.
Wakili anayemtetea Lulu akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mteja wake kupata dhamana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo. Lulu amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali waliosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja, kusalimisha hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam  bila ruhusa ya mahakama na kuripoti kwa msajili kila mwezi.  Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba
Endelea Kusoma >>
0 comments

WASHINDI WA DROO YA AMKA MILIONEA WAPATIKANA


Meneja uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando( kulia)  akiongea na washindi wa promosheni ya Amka millionea wakati wa droo ya wiki ya sita ya promosheni hiyo ambapo wateja mbalimbali wa Airtel wameibuka washindi wa pesa taslim, katika ni Afisa huduma za ziada wa Airtel Fatma Ngororo na kushoto ni Mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Bi Chiku Saleh, Jinsi ya kushiriki promosheni hiyo mteja atatakiwa kutuma neno SHINDA au WIN kwenda namba 15595 bure na atapokea maswali atakayoyajibu na kukatwa sh 350 kila sms na kupata point zitakazomuwezesha kushinda  kila siku za sh milioni 1 au 2 na kila mwisho wa mwizi   shilingi milioni  15Tsh.
 
Endelea Kusoma >>

KABANGE TWITE HATOCHEZA YANGA MSIMU HUU WA LIGI KUU INAYOENDELEA KUSUBIRI MSIMU UJAO

0 comments




Mchezaji Alain Kabange Twite hataweza kuichezea Yanga msimu huu (2012/2013) baada ya klabu hiyo kuingiza nyaraka zenye upungufu wakati ikimuombea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa njia ya mtandao (Transfer Matching System- TMS).



Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), baadhi ya nyaraka zenye upungufu katika maombi hayo ni mkataba kati ya Twite na Yanga, lakini vile vile makubaliano ya mkopo (Loan Agreement) kati ya Yanga na FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ambayo ndiyo inayommiliki mchezaji huyo.



Ili mchezaji aweze kupata ITC kwa njia ya TMS, kwa mujibu wa Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za TFF kuna nyaraka kadhaa muhimu zinatakiwa kukamilika katika maombi hayo ili hati hiyo iweze kupatikana.



AZAM YAIFUKUZIA YANGA VPL

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya 15 kesho (Januari 30 mwaka huu) kwa mechi mbili ambapo Azam iliyo katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga itakuwa mwenyeji wa Toto Africans ya Mwanza.



Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam huku Azam ikisaka ushindi ili kuikaribia Yanga inayoongoza wakati Toto Africans inayonolewa na John Tegete ikitaka kurekebisha makosa ya kupoteza mechi yake iliyopita dhidi ya Oljoro JKT.



Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Oljoro JKT dhidi ya wageni Kagera Sugar kutoka Bukoba mkoani Kagera itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo wa Musoma.



Ushindi kwa Oljoro JKT yenye pointi 17 utaihakikishia kubaki katika nafasi yake ya nane wakati Kagera Sugar inayofundishwa na kocha mkongwe Abdallah Kibaden utaifanya ipige hatua moja mbele katika msimamo wa ligi.



Ligi itaendelea tena Jumamosi (Februari 2 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo vinara Yanga wataumana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Polisi Morogoro ikiikaribisha African Lyon mjini Morogoro.



Nazo Mgambo Shooting ya Tanga na Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.



KAMPUNI TANO ZAOMBA KUKARABATI HOSTELI TFF

Kampuni tano zimewasilisha tenda zao kuomba kupewa kazi ya kukarabati hosteli ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Januari 7 mwaka huu TFF ilitangaza tenda kwa ajili ya ukarabati wa hosteli hiyo baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kukubali ombi lake la kutoa fedha kwa ajili ya kazi hiyo.



Ufunguzi wa tenda hizo ulifanyika jana (Januari 28 mwaka huu) kupitia kwa Bodi ya Tenda ya TFF mbele ya wazabuni wote watano waliowasilisha tenda zao na kushuhudiwa pia na Mkandarasi mshauri. Wazabuni (kampuni) waliojitokeza awali walikuwa saba, lakini waliorejesha zabuni zao ni watano.



Kampuni hizo ni Crescent Concrete Limited, DGS Company Limited, Mart Builders Company Limited, Prince General Investment Limited na Send Star Company Limited.



Bodi ya Tenda ya TFF itakutana Januari 31 mwaka huu pamoja na mambo mengine kuchagua kampuni ambayo itafanya ukarabati huo.



LALA SALAMA DARAJA LA KWANZA KUANZA JUMAMOSI

Mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambayo itatoa timu tatu zitakazocheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao (2013/2014) unaanza Jumamosi (Februari 2 mwaka huu) katika viwanja tisa tofauti.



Kundi A litakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Burkina Faso itakayochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Majimaji na Kurugenzi katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea, na Polisi Iringa dhidi ya Mkamba Rangers kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.



Mechi za Kundi B, Jumamosi (Februari 2 mwaka huu) itakuwa Transit Camp na Ndanda itakayochezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, Moro United dhidi ya Villa Squad (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam). Jumapili (Februari 3 mwaka huu) ni Tessema na Green Warriors (Mabatini, Pwani), Ashanti United na Polisi Dar (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam).



Kundi C Jumamosi (Februari 2 mwaka huu) ni Polisi Dodoma na Kanembwa JKT (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Morani dhidi ya Mwadui (Uwanja wa Kiteto, Manyara), Polisi Mara na Pamba (Uwanja wa Karume, Musoma), Polisi Tabora na Rhino Rangers (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).



Ligi hiyo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Machi mwaka huu ambapo mshindi wa kila kundi atapanda daraja kucheza Ligi Kuu msimu ujao. (Ratiba imeambatanishwa)



WAPAMBE MARUFUKU KWENYE PINGAMIZI, USAILI TFF

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesema waliowekewa pingamizi na wa walioweka pingamizi hawaruhusiwi kufika katika kikao cha kesho (Januari 30 mwaka huu) wakiwa na vikundi vya ushangiliaji au wapambe.



Kikao cha kupitia pingamizi kitafanyika saa 4 asubuhi na wapambe au washabiki wa waombaji uongozi pamoja na waweka pingamizi hawakiwi kuwepo kwenye eneo la kikao hicho.



Wote walioweka pingamizi na waliowekewa pingamizi barua zao za mwito wa kuhudhuria kikao cha  Kamati ya Uchaguzi ya TFF zimeshatumwa kwenye anwani za barua-pepe zilizo kwenye taarifa za pingamizi au kwenye fomu za maombi ya uongozi.



Leo waombaji uongozi watatumiwa barua za mwito kwa barua-pepe wa kuhudhuria usaili utakaofanyika tarehe 01-02 Februari 2013. Tarehe 01 Februari 2013 watasailiwa waombaji uongozi wa TPL Board na waombaji ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia Kanda ya 1 hadi Kanda ya 8. Waombaji uongozi kupitia Kanda ya 9 hadi ya 13 na waombaji uongozi wa Makamu wa Rais na Rais wa TFF watasailiwa tarehe 02 Februari 2013 kuanzia saa 4 asubuhi.



Vyombo vingi vya habari vimeonyesha nia ya kuwepo mdahalo wa wagombea uongozi katika TPL Board na TFF. Kanuni za Uchaguzi za TFF hazizuii jambo hilo kufanyika, bali tu lizingatie Kanuni za Uchaguzi za TFF. Mojawapo ya mambo ya kuzingatiwa ni kwamba mdahalo huo ufanyike wakati wa kipindi cha Kampeni na usiwe na taswira ya kuwapendelea au kuwabagua baadhi ya wagombea. Kanuni hazimlazimishi mgombea kushiriki mdahalo.



Pia ni vema mdahalo ukaandaliwa na kuratibiwa  na Taasisi inayounganisha vyombo vya habari au waandishi wa habari kama TASWA. Kamati ya Uchaguzi ya TFF lazima ijulishwe kwa maandishi nia hiyo ya kufanyika mdahalo na utaratibu utakaotumika mapema kabla ya kufanyika mdahalo huo ili kujiridhisha kuwa utaratibu utakaotumika kuandaa na kuendesha mdahalo haukiuki kanuni za Uchaguzi za TFF.



Kamati ya Uchaguzi ya TFF inavishukuru vyombo vya habari kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi hadi sasa na kuwaomba waendelee kufanya hivyo hadi mwisho wa mchakato wa uchaguzi.



Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Endelea Kusoma >>

picha za matukio ya Kigoma na ccm

0 comments
  Dk. Asha Rose Migiro akishangiliwa na mkazi wa Nguruka, Asha Kipenda wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana na ujumbe wake.jpg7. Dk. Asha Rose Migiro akishangiliwa na mkazi wa Nguruka, Asha Kipenda wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana na ujumbe wake.jpg


 Juma Kilabuka na Hasani Kankwi wa mjini mdogo wa Nguruka wakifurahia msafara wa Kinana ulipofika katika mji huo.huku wakiwa na mifugo yao yambuzi wakimpa dole katibu mkuu kinana kufika katika mji wao
Badhi ya wakazi wa mji mdogo Nguruka Wilayani Uvinza  wakifuatili kwa makini mkutano ulikuwa unahutubiwa na katibu mkuu wa ccm Abdulrahamani kinana 


 . Kinamama katika mji mdogo wa Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma, wakipokea kwa shangwe msafara wa Kinana na ujumbe wake ulipowasili kwa ajili ya mkutano wa hadhara


 Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Sik You, (wapili kushoto) akiwatembeza Kinana (watatu kushoto), Migiro (wanne) na Nape (wapili kushoto) .jpg1. Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Sik You, (wapili kushoto) akiwatembeza Kinana (watatu kushoto), Migiro (wanne) na Nape (wapili kushoto) .jpg
Endelea Kusoma >>
0 comments
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo, wanaowakilisha makundi mbalimbali ya vijana. Picha na OMR
Endelea Kusoma >>

Monday, January 28, 2013

0 comments

*LULU AKIREJEA RUMANDE BAADA YA MSAJILI WA MAHAKAMA KUTOKUWEPO OFISINI LEO KUKAMILISHA TARATIBU ZA DHAMANA YAKE.


 Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo baada ya Msajili wa Mahakama Kuu kutokuwepo ofisini na hivyo kurudi rumande hadi kesho tarehe 29/1/2013 atakapoletwa kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhamana ikiwa ni pamoja na kusalimisha  kwa Msajili wa mahakama hiyo hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es Salaam  bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa msajili kila tarehe 1 ya kila mwezi, kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali  ambao watasaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja. Lulu anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba. 
Gari lililomleta Lulu likiondoka mahakamani hapo.
Lulu akisindikizwa na askari Magereza. 
Lulu akipanda katika gari la Magereza kurudi Rumande, baada ya kukamilisha taratibu za dhamana hiyo na kukosekana kwa Msajili wa Mahakama Kuu, mahakamani hapo. Picha na Habari Mseto
Endelea Kusoma >>

RAI KIKWETE AWASILI NYUMBANI KUTOKA ETHIOPIA

0 comments
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik Muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jana usiku akitokea nchini Ethiopia ambapo aluhudhuria mkutano wa Wakuu wan chi za umoja wa Afrika(AU) uliofanyika jijini Addis Ababa(picha na Freddy Maro)
Endelea Kusoma >>

YANGA, TANZANIA PRISONS WAINGIZA MIL 101

0 comments



Yanga na Tanzania Prisons zimeingiza mapato ya jumla ya sh. 101,016,000 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara iliyofanyika jana (Januari 28 mwaka huu).



Mechi hiyo namba 94 ilichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Watazamaji 17,946 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.



Watazamaji 16,158 kati ya hao walikata tiketi za sh. 5,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ni 98 waliokata tiketi za sh. 20,000.



Kila klabu imepata mgawo wa sh. 24,314,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,409,220.34. Asilimia 15 iliyokwenda kwenye uwanja baada ya kuondoa VAT na gharama za tiketi ni sh. 12,363,433.45.



Mgawo mwingine wa mapato hayo ni tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 7,413,060.07, Kamati ya Ligi sh. 7,418,060.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,709,030.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,884,801.14.



Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Endelea Kusoma >>
0 comments
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA

WIZARA ITASHIRIKIANA NA WADAU KUTATUA MIGOGORO YA UHIFADHI WILAYANI LOLIONDO

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Khamis Kagasheki amewataka wananchi na wadau wote wanaoishi katika Wilaya ya Loliondo kushirikiana na Serikali katika mchakato wake wa kutatua migogoro ya ardhi inayohusiana na uhifadhi wilayani humo.
Waziri Kagasheki aliyasema hayo jana akiwa Loliondo katika mkutano kati yake na wawakilishi wa wananchi, Mashirika yasiyo ya Serikali, na Wawekezaji. Waziri Kagasheki alifanya ziara ya siku noja wilayani Loliondo ili kuzijua kero zilizopo kati ya wadau kuhusiana na mipaka ya hifadhi.
Katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na Mbunge wa Ngorongoro Mhe Kaika Ole Telele, ilielezwa kuwa baadhi ya kero ni kuwa mapato yanayotolewa na Kampuni ya Uwindaji ya OBC kwa wananchi hayatoshi, hivyo yaongezwe.
Ilielezwa pia kuwa Kampuni ya Thompson Safaris inamiliki eneo ambalo ni vyanzo vya maji ambayo yanahitajiwa na wananchi wa vijiji vitatu vilivyoko wilayani humo, hivyo eneo hilo liwe huru kutumiwa na wadau wote.
Vilevile kulikuwa na malalamiko kutoka kijiji cha Ololosokwan kuwa wakati wa kupima mipaka na kuweka maboya eneo la kijiji hicho lilimegwa na TANAPA na Hifadhi ya Ngorongoro.
Aidha Madiwani wa Loliondo waliomba kuwa eneo ambalo linasimamiwa na Idara ya Wanyamapori libadilishwe matumizi ili lisimamiwe na wananchi kama Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori (WMA).
Baada ya kusikiliza kero za wadau Mhe Kagasheki alisema kuwa matatizo ya Loliondo yanayohusiana na uhifadhi sharti yatatuliwe, lakini utatuzi wake lazima ufuate sheria na busara. Alisema kuwa kutumia busara ni muhimu kwa kuwa kuna watu ambao wameishi katika baadhi ya maeneo yanayosemekana kuwa ni ya migogoro kwa muda wa miaka 40 hadi sasa.
Waziri Kagasheki alisema kuwa atafanya kazi kwa karibu na Mbunge wa Ngorongoro Mhe Kaika Ole Telele pamoja na wadau wengine ili muafaka uweze kufikiwa haraka iwezekanavyo.
Kwa upande mwingine, Waziri Kagasheki alizitaka Taasisi Zisizo za Serikali (NGOs) kuchangia katika kuleta muafaka badala ya kuchochea kutoelewana kati ya Serikali na Wananchi.
Pia Waziri Kagasheki aliwataka wawekezaji kuunda umoja ali waweze kujadili changamoto zilizopo na kuzitafutia uvumbuzi kwa pamoja badala ya kuwagawa wananchi. Aliwahimiza washirikiane na Halimashauri ya Wilaya na kuwa  misaada wanayotoa kwa wananchi inatakiwa iwekwe wazi.

[MWISHO]

George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA  MALIASILI NA UTALII
28 Januari 2013

Simu 0784 468047

Endelea Kusoma >>

Sunday, January 27, 2013

0 comments

NYAMLANI, MALINZI , WAMBURA WAWEKEWA PINGAMIZI TFF

 Katibu Mkuu wa TFF na Kamati ya Uchaguzi, Angetile Osiah  *** UCHAGUZI WA VIONGOZI WASHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) NATANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD (TPL BOARD)27101/2013 Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawataarifu wadau wa soka kuwa fursa ya kuweka pingamizi kwa wagornbea uongozi wa TFF na Tanzania Premier League Board (TPL Board) ilìkwisha jana tarehe 26 Januari 2013 Saa 10.00 jioni. Kamatí ya uchaguzi ilipokea pingamìzi kwa waombaji.
Endelea Kusoma >>

FRANK DOMAYO TAABANI AUGUA GHAFLA NA KUENGULIWA KIKOSI YANGA LEO UWANJANI

0 comments


Kiungo wa Yanga, Frank Domayo akiwa amelala katika zahanati ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mida hii, baada ya kupatwa na Malaria ya ghafla. Domayo ilikuwa aanze mechi ya leo, lakini kutokana na kuugua huko ghafla, sasa nafasi yake ataanza Nurdin Bakari.

Kiungo wa Yanga, Frank Domayo akiwa amelala katika zahanati ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mida hii, baada ya kupatwa na Malaria ya ghafla. Domayo ilikuwa aanze mechi ya leo, lakini kutokana na kuugua huko ghafla, sasa nafasi yake ataanza Nurdin Bakari.
Endelea Kusoma >>

BREMKING NEWZZZ LOWASA APATA AJALI ATT MACOMRADE MH LOWASSA AMEPATA AJALI LKN YUKO SALAMA NAWAPA HIZO TIPS KIDOGO, ZAIDI NIPIGIENI 0655685085

0 comments
PICHA ZA GARI LA MZEE LILILOPATA AJALI. DEREVA ANAITWA YANGA ANASTAHILI SIFA ZA PEKEE KWA KWELI ALIFANYA KAZI KUBWA KUMKWEPESHA MZEE NA AJALI MBAYA KABISA

ATT MACOMRADE MH LOWASSA AMEPATA AJALI LKN YUKO SALAMA NAWAPA HIZO TIPS KIDOGO, ZAIDI NIPIGIENI  0655685085

waziri mkuu mstaafu na mbunge wa monduli edward lowassa amenusurika kifo, baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupata ajali eneo la bwawani mkoani morogoro.
Gari hilo la mh lowassa liligongwa na basi la morobest, wakati basi hilo lilipolipita basi jingine kwenye daraja na kukutana uso kwa uso na gari la mh.Lakini dereva wa mzee kwa ustadi mkubwa alilikwepesha gari lisigonge upande alipokuwa amekaa  mzee na kuligonga ubavuni nyuma kwa upande wa dereva. hakuna aliyejeruhiwa.Lowassa na msafara wake aliendelea na safafrti hadi morogoro ambako ameshiriki katika harambee ya ujenzi wa kanisa la kkkt kilakala.

akizungumzia ajali hiyo, lowassa amesema mkono wa mungu ni mkubwa, bila ya hivyo  simulizi zingekuwa nyingine juu yake.pia alisema kuwa wakati alipoliona basi likiwa linakuja upande wake kuwagonga, ukamjia wimbo mmoja wa dini unaonesema kuwa ''hivi haya yote ya nini, ni huruma tu''.


Endelea Kusoma >>
0 comments

APIGWA RISASI KWA UGOMVI WA SH. MIA MOJA

 
 
 
 
 
 
 MKAZI wa mtaa wa Tandika,Frank Filias (25) akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya Temeke wodi namba saba baada ya kupigiwa risasi na mfanyabiashara mmoja wa mbao kufuatia ugomvi wa kudaiana Sh 100 ya maji ambayo mama yake mzazi, Sarah Mwaikatale alidaiwa na jirani yake kuwa alishindwa kumlipa (Picha Na Christopher Nyenyembe )
Endelea Kusoma >>

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akifurahi na mitoto Ali Saidi

0 comments


 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akimfurahia mtoto Ali Saidi mwenye umri wa miezi minane, ambaye ni mtoto wa  mmoja wa abiria aliowakuta kwenye  Stesheni ya Kigoma, msafara wa Kinana ulipowasili leo kwa treni.Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.






 Abiria wakiwa katika behewa la daraja la watatu, wakitoka Tabora kwenda Kigoma leo
Endelea Kusoma >>

ASHA ROSE MIGIRO,KINANA NA NAPE WAKIPATA MISOSI YA USWAZI

0 comments
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinunua mishikaki kwa mmoja wa wauzaji wa vyakula mbalimbali husuasan nyama, baada ya kuwasili na msafara wake stesheni ya Saranda, mkoani Singida, leo mchana. Kinana na msafara wake wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, wanasafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam, kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM. (Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai. 

Makatibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia) na wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kulia) wakinunua chakula kwa mamalishe, kwenye stendi ya Saranda mkoani Singida, daaba ya kuwasili kwenye stesheni hiyo, Wakati Msafara wa Sekretarieti ya CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ulipokuwa katika safari yake kwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwenye sherehe za miaka 36 ya CCM.(Picha na Bashir Nkoromo)

Endelea Kusoma >>

MBUNGE WA MOROGORO AKITEMBELEA BWAWA LA MINDU

0 comments
mbunge wa jimbo la morogoro mjini Abdullazizi Abood akitembelea draja
DHI ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro,wameupongeza utendaji kazi wa Mbunge wa jimbo lao Abdulaziz Abood,(CCM)kutokana na kufanya ziara za kustukiza katika maeneo yanayolalamikiwa na wananchi.

Miungoni mwa maoneo yaliyolalmikiwa siku za hivi karibuni ni pamoja na maji yanayosambazwa na mamlaka ya maji safi na maji taka yanayotoka katika mabomba kuwa machafu ambapo Mbunge huyo alifanya ziara ya kustukiza katika bwa la mindu na kuagiza uongozi wake kurekebisha hali hiyo kitu ambacho kilifanyika.
Eneo lingine ni pamoja na Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambapo wanachi walilalamikia huduma duni na lugha chafu zinazotolewa na wauguzi kwa wagonjwa na Mbunge huyo kulazimika kufika katika eneo hilo na kushuudia hali hiyo baada ya kuelezwa na wagonjwa walilazwa katika  wodi mbalimbali.
Hata hivyo kufuatia hali hiyo ilimlazimu Mbunge huyo  kuzungumza na uongozi wa Hospitali hiyo ili waweze kukemea wauguzi wenye tabia hiyo kwani wagonjwa wanahitaji kupewa faraja.
Wakizungumza na Waandishi habari  mjini hapa ,wanachi hao wanaoishi maeneo ya kihonda walisema katika kipindi cha takribani mwezi mmoja mamlaka ya majisafi na maji taka Moruwasa bila huruma imekuwa ikiwanywesha maji machafu yenye rangi ya kijani,yanayowasha na yanayotoa povu pindi wanapoyachemsha.
“Nampongeza Abood kwa ziara yake maana zaidi ya mwezi mmoja wananchi tulikuwa tunakunywa  maji machafu kupita kiasi hadi kubadilika kuwa na rangi ya kijani na ukiyachemsha yanatoa povu kama maji ya kufulia nguo sasa amejionea uhalali wa malalamiko ya wananchi kuhusu tatizo hili la maji”. alisema Agnes Julius  mkazi wa  kihonda Magorofani.
Naye  Ramadhani Omary  mkazi wa Kichangani alisema kuwa utendaji wake umesaidia kutatua kero katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako wauguzi wamekuwa wakitoa lugha chafu kwa wagonjwa.
Kwa upande wake Abood alisema kuwa yeye amechaguliwa na wananchi hivyo atahakikisha anatetea na kupigania maslahi ya yao huku akisisitiza kumpa ushirikiano kuweza kufikia malengo hayo.
“ Mimi nimegombea ubunge kwajili ya kutetea maslahi ya wananchi wa Morogoro,hivyo siku zote nitakuwa upande wao “ alisema Abood.
Mwisho

Endelea Kusoma >>
0 comments
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116539 
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website:  www.mawasilianoikulu.go.tz  
Fax: 255-22-2113425
        
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
       P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
    
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
·        Mradi kabambe wa umeme kujengwa
·        Rais Kikwete apokea ripoti ya maandalizi
·        Utagharimu mabilioni ya fedha
·        Utaunganisha mikoa yote kwenye Gridi ya Taifa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Oktoba 12, 2011, amepokea ripoti kutoka makampuni mawili ya kimataifa kuhusu Mpango Kabambe ya mradi mkubwa wa umeme ambao utaunganisha kwenye Gridi ya Taifa mikoa yote sita ambayo kwa sasa haiko kwenye gridi hiyo.

Rais Kikwete amepokea ripoti hiyo kutoka makampuni ya China National Machinery&Equipment Import&Export Corporation (CMEC) ya China na Siemens ya Ujerumani ambayo kwa pamoja yanatarajia kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 1,100 kutoka Mtwara hadi Singida.

Mradi huo mkubwa wa umeme wa megawati 300 utakaogharimu karibu dola za Marekani milioni 684 na utakaozalisha umeme wa moja kwa moja na wenye nguvu kubwa ya 300 kV (300 kV High Voltage Direct Current – HVDC) utagharimiwa kwa pamoja na mkopo kutoka Benki ya Exim ya China na Serikali ya Tanzania.
Umeme kutokana na mradi huo utaunganishwa kwenye gridi ya taifa na kutoka Singida hatimaye utavutwa kupelekwa katika mikoa ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ya Kagera, Kigoma na Rukwa ambako pia utaongeza upatikanaji wa umeme katika machimbo ya madini yaliyoko katika mikoa hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mbali na mikoa hiyo mitatu, pia mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo nayo haiko katika Gridi ya Taifa nayo itaunganishwa katika Gridi hiyo kupitia umeme huo.
Kuunganishwa kwa mikoa hiyo sita katika Gridi ya Taifa kupitia umeme wa mradi huo pamoja na Mkoa wa Ruvuma ambao utaunganishwa katika Gridi hiyo kwa mradi unaogharimiwa na Serikali ya Sweden kutakamilisha mpango wa Serikali ya Awamu ya Nne kuunganisha mikoa yote ya Tanzania kwenye umeme wa Gridi ya Taifa.
Kwa sasa Mkoa wa Kagera unahudumiwa na umeme kutoka Uganda, wakati Mikoa ya Kigoma na Rukwa inahudumiwa na umeme wa mafuta ya dizeli. Mikoa ya Mtwara na Lindi inapata umeme wake kutoka kampuni ya Wentworth ambao haujaunganishwa kwenye gridi ya taifa.
 Kuunganisha mikoa yote ya Tanzania kwenye Gridi ya Taifa ilikuwa moja ya ahadi kubwa zilizotolewa na Serikali ya Rais Kikwete wakati anaingia maradakani na kwa kuuunganisha mikoa hiyo sita kwenye Gridi hiyo, Serikali hiyo itakuwa imetimimiza ahadi hiyo.
Akipokea ripoti hiyo, Rais Kikwete ameishukuru Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa juhudi zao zilizofanikisha makubaliano ya kujengwa kwa mradi huo mkubwa wa umeme ambao utachangia kuongeza wingi wa umeme nchini katika kipindi ambacho kwa miezi kadhaa Tanzania imekabiliwa na mgawo wa umeme kutokana na ukame uliokausha maji kwenye mabwawa makubwa ya uzalishaji umeme nchini.
Rais Kikwete pia ameitaka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki ya EXIM ya China kuhakikisha kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zinapatikana haraka iwezekanavyo na pia ameitaka TANESCO na makampuni ya CMEC na Siemens baada ya kupatikana kwa fedha kuanza ujenzi wa mradi huo kwa kasi na kuukamilisha katika muda na ubora unaotarajiwa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Endelea Kusoma >>

TAARIFA YA NDUGU ZITTO KABWE (MB) KUHUSU YANAYOENDELEA MTWARA NA MRADI WA BOMBA LA GESI ASILIA

0 comments




Serikali iache kutafuta mchawi, iende Mtwara

Katika kipindi cha wiki nne sasa kumekuwa na maandamamo, malumbano na vurugu kuhusu mradi wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Mradi huu wa kutandaza bomba la urefu wa kilometa 542 ni mkubwa sana hapa nchini, na una thamani kubwa zaidi kuliko miradi mingine yote  ya miundombinu iliyopata kutokea hapa nchini. Mradi huu utajengwa kwa mkopo wa dola za Kimarekani 1.2 bilioni kutoka Benki ya Exim ya China.

Wananchi wa Mtwara kupitia maandamano ya tarehe 27 Desemba 2012 wametaka kujua hatma ya maendeleo ya mikoa wa kusini kutokana na mradi huu wa bomba la gesi. Serikali imewajibu wananchi hawa kwa kuwaita wahaini, watu hatari na wasio elewa. Imefika mahali inapotosha madai yao kwamba hawataki gesi itoke Mtwara.

Kimsingi Serikali haijajibu hoja yeyote ya msingi ya wananchi wa Mtwara kuhusu mradi wa kusafirisha gesi. Badala yake imekuwa ikijaribu kupotosha madai ya watu wa Mtwara kupitia mikutano na vyombo vya habari.

Tangu maandamano haya yatokee, na baadaye mikutano ya hadhara na
hatimaye matukio ya kusikitisha ya kuharibu mali za watu, mauaji ya
watu na majeruhi mbalimbli, Serikali na hasa Wizara yenye dhamana ya
mradi huu, imekuwa ikitoa matamko kwenye vyombo vya habari badala ya
kwenda Mtwara kuzungumza na wananchi, kusikiliza madai yao na kuona
namna ya kutekeleza madai hayo. Kutokana na Serikali kutofanya hivyo,
kusikiliza na kuzungumza na wananchi wa Mtwara, vurugu mbaya sana zimeendelea mkoani humo.

Mwezi uliopita, Desemba 2012, tatizo lilionekana kuwa ndogo na lenye kuhusiana zaidi na ukosefu wa kushirikishwa kwa wananchi. Badala ya kushughulikia
tatizo likiwa bado ndogo, Serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisemakuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro
huu.

Leo hali iliyopo mkoani Mtwara inasikitisha sana, maana mali za wananchi zinaharibiwa, nyumba zinachomwa moto na watu wanapoteza maisha. Tunalaani matukio haya kwa nguvu zetu zote, maana kinachotokea Mtwara si Utanzania. Tusipowasikiliza wananchi na kutatua mgogoro huu kwa kuwashirikisha, hali itazidi kuzorota wakati tukitupiana lawama.

Hivi sasa serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisema kuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro huu.

Kwanza, Serikali imekuwa ikiaminisha umma kwanza suala hili limechukuliwa kisiasa. Pili, Serikali imekuwa ikirudia kusema kuwa baadhi ya makampuni ya uwekezaji nchini na mataifa ya Magharibi yamekuwa yakichochea wananchi wa Mtwara.

Katika mwendelezo wa mtindo wa Serikali wa ‘management by press conferences’ jana Jumamosi Naibu Waziri wa Nishati na Madini ndugu George Simbachawene aliwaambia wahariri kwamba mimi Zitto Kabwe ninachochea wananchi wa Mtwara, ninatumiwa, na si mzalendo. Vile vile alitoa vielelezo kadhaa kuonyesha kuwa mradi wa kujenga bomba la gesi ni gharama sawasawa. Akasisitiza kwamba mimi ni mwongo.

Katika kipindi chote cha mgogoro wa Gesi Mtwara, sijafika Mtwara. Sijafanya mkutano wowote na waandishi zaidi ya kuandika mawazo yangu, kama Mtanzania kuhusu suala hili.

Nimeandika makala nne na zimechapishwa katika magazeti kadhaa hapa nchini na kwenye blogu yangu (http://zittokabwe.wordpress.com/).

Niliandika: Utajiri wa Gesi Asilia: Tuwasikilize Watanzania wa Mtwara na Lindi. Nikaandika tena: Tusipuuze mandamano dhidi ya Bomba la Gesi: Kilio cha Uwajibikaji; Nikaandika tena: Mtwara : Serikali inavunja nchi kwa kutosikiliza Wananchi; ni baadhi ya makala nilizoandika kuhusiana na suala la Mtwara.

Sitaki kubishana na Naibu Waziri ama Kiongozi yeyote ya Serikali kwa sasa. Hatuwezi kuendelea kulumbana, kuzozana, kuzodoana na kurushiana maneno wakati nchi yetu inaungua. Huu sio wakati wa kutafuta mchawi bali kutafuta majawabu ya changamoto zilizopo mbele yetu.

Yanayotokea Mtwara ni fundisho kwetu kwa Taifa namna ya kukabili changamoto za utajiri wa rasilimali, ili kuweka mkakati, mambo haya yanayotokea Mtwara yasitokee tena Tanzania. Tutaweza kuzuia maafa haya iwapo tutaweka uwazi katika mikataba, tutashirikisha wananchi kwenye unyonyaji wa maliasili za nchi, na iwapo tutaweka uwajibikaji.


Rais Kikwete Kikwete ana majibu; ayatoe sasa kwa wana Mtwara

Kwa mujibu wa Mpango Kabambe wa Umeme nchini (Power System Master Plan), kulikuwa na mradi wa kufua umeme MnaziBay, ambao Rais Jakaya Kikwete aliagiza utekelezwe mara moja. Serikali ieleze umma kuhusu mradi huo wa kujenga kituo cha kufua umeme 300MW MnaziBay Mtwara na kujenga msongo wa umeme wa 300KV mpaka Singida. Umeishia wapi? Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 12 Oktoba 2012, Rais Jakaya Kikwete alipokea ripoti ya ujenzi wa mradi huu kutoka makampuni ya China National Machinery & Equipment Import & Export Corporation (CMEC) ya China na Siemens ya Ujerumani, ambayo kwa pamoja yalitarajia kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 1,100 kutoka Mtwara hadi Singida. Mradi huu ungegarimu dola za kimarekani milioni 684 na Rais aliagiza utekelezwe haraka sana. Huu mradi uliishia wapi? Kwa nini Serikali ipo kimya kuhusu mradi huu ambao ungejibu kabisa maswali ya watu wa Mtwara? Taarifa ya Ikulu kuhusu mradi huu imeambatanishwa hapa.

Tufanyeje?

Hapa tulipofikia ni lazima kwanza kabisa kusikia kilio cha wananchi wa Mtwara ikiwemo kuelewa madai yao. Swali kubwa kubwa la watu wa Mtwara na Kusini kwa ujumla ni ‘tunanufaikaje’? Jibu la swali hili si ahadi za miradi bali ni vitendo. Hapa ndipo serikali inaposhindwa kushughulikia suala hili, kutoelewa madai ya wananchi na kuyapotosha.Viongozi wa kisiasa wenye ushawishi kutoka pande zote, chama tawala na vyama vya upinzani, waende Mtwara kuzungumza na wananchi, lakini wawasikilize kwanza.

1.    Lazima viongozi tujenge utamaduni wa kusikiliza wananchi na si kuwahutubia tu. Wananchi wa Mtwara wana madai ambayo lazima viongozi tukae kitako kuwasikiliza kisha kufanya nao majadiliano ambayo yatatoa mwafaka. Rais mstaafu, Ndugu Benjamin Mkapa ameshatoa kauli kuhusu suala hili. Ni wakati mwafaka sasa kwa viogozi wengine kumuunga mkono kwa kwenda Mtwara na kukaa na wananchi wa Wilaya zote za Mtwara, kusikiliza hoja zao na kuona namna ya kupata ufumbuzi wa suala hili. Wakati hatua hii inachukuliwa, wananchi waombwe kutulia na kuacha vurugu za aina yeyote ile, na Serikali isimamishe mradi mpaka hapo suluhu na wananchi itakapopatikana.

2.    Wakati juhudi hizo zinaendelea Serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi wa bomba, kwani ni dhahiri gharama za mradi huu ni kubwa mno kulingana na uhalisia wa miradi ya namna hii duniani kote. Katika taarifa zote kwa umma Serikali imekuwa ikisema kwamba mradi utagharimu jumla ya dola za kimarekani 1.2 bilioni, lakini katika taarifa ambayo Wizara ya Nishati na Madini imesambaza jana kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini imesema mradi utagharimu dola za kimarekani milioni 875. Usiri katika mkataba huu unaashiria kwamba Serikali inaficha kitu. Hivyo njia pekee ni kutaka mkataba uwe wazi kwa wananchi.

3.    Wakati tunawataka wananchi wa Mtwara kuruhusu utulivu, ni vema Serikali ijiandae kutoa majawabu ya madai ya wananchi hao. Majawabu ya Serikali yajikite kueleza wananchi wa Mtwara wanafaidikaje na rasilimali ya gesi asilia kwa maendeleo yao. Wananchi wa Mtwara wanataka uwajibikaji wa Serikali kwenye utajiri wa nchi, na wamechoka na porojo za orodha ya miradi isiyotekelezwa.

Viongozi twendeni Mtwara kusikiliza wananchi wetu. Nchi inaungua na hatuwezi kuendelea kuzozana badala ya kuzima moto huu hatari kama vita vya MajiMaji. Mimi nakwenda Mtwara haraka na mara baada ya viongozi wangu wa chama kutoa ridhaa.


ZITTO KABWE
Mbunge, Kigoma Mjini (Chadema)
Waziri Kivuli wa Fedha
Endelea Kusoma >>
 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu